Usikate Tamaa ya Kuomba,Omba mpaka Litokee
Hata kama Lipo jambo ambalo umeliombea Muda Mrefu na bado hujapata Majibu,Ujumbe wa Leo kwako; Usikate Tamaa ya Kuomba, Omba mpaka litokee. (Jifunze hapa Kwa Eliya alipokuwa anaomba Mungu ili mvua inyeshe katika Nchi). Mara ya kwanza,hakuna kitu,akaendelea;baadae(mara ya 7) mazingira yakaanza kubadilika na MVUA ikanyesha Nyingi.
Eliya alipopanda juu mpaka kilele cha Mlima Karmeli; alisujudu kifudifudi, akainama uso mpaka magotini.
Akamwambia mtumishi wake, Kwea sasa, utazame upande wa bahari. Akakwea, akatazama, na kusema, Hakuna kitu. Naye akanena, Enenda tena mara saba.
Ikawa mara ya saba akasema, Tazama, wingu linatoka katika bahari, nalo ni dogo kama mkono wa mtu. Akanena, Enenda, umwambie Ahabu, Tandika, ushuke, mvua isikuzuie.
Ikawa, muda si muda, mbingu zikawa nyeusi kwa mawingu na upepo, ikanyesha mvua nyingi. Ahabu akapanda garini, akaenda zake Yezreeli.(1 Wafalme 18-42-45).









image quote pre code