Ugonjwa Wa Tezi Dume,Chanzo,Dalili na Tiba
Kila mwanaume anazaliwa na Tezi ya kiume. Tezi dume siyo ugonjwa bali ni kiungo kama viungo vingine mwilini. Tezi dume inapatikana katika mfumo wa uzazi wa mwanaume katika shingo ya kibofu cha mkojo. Kazi yake kubwa nikutengeneza majimaji ya uzazi kwa mwanaume ambayo husaidia kurutubisha mbegu za kiume zilizo tengenezwa kutoka kwenye Korodani; na husaidia mbegu za kiume kubaki hai kwa muda unaostahili.
Tatizo linakuja pale kiungo hiki kinapoanza kutanuka. Kiungo hiki kinatanuka taratibu taratibu mnoo. Hili ni tatizo linalo wakumba wanaume wengi.
UKUAJI WA TEZI DUME
Ukuwaji wa Tezi dume ni ile hali ya chembe chembe hai katika tezi ya kiume kukua bila kufuata utaratibu wa mfumo wa mwili katika eneo linalo zunguka mirija ya kupitisha mkojo na mbegu za kiume.
Tatizo hili kwa sasa linawapata wanaume kuanzia umri wa miaka 25 na kuendelea, tofauti na awali ilikuwa umri mkubwa miaka zaidi ya 50.
Takwimu kutoka kwenye shirika la CHRP (Centre for Human Right Promotion), zinaonesha kwamba kiujumla kila mwanaume katika maisha yake ana 16% za kugundulika saratani ya Tezi Dume, Na Saratani hii inaua mwanaume mmoja kila baada ya dakika 13.
• Soma: Tatizo la Mapunye Kichwani kwa Watoto wadogo
VYANZO VINAVYOPELEKEA TEZI DUME KUTANUKA
Tatizo la kutanuka kwa tezi dume limekuwa kwa kasi sana hii ni kutokana na mitindo ya maisha wanaume wengi wanayoishi.
Vifuatavyo ni vitu vinavyoongeza hatari ya kutanuka kwa tezi dume:
- Ukosefu wa lishe kamili na upungufu wa Virutubisho muhimu mwilini
- Uwepo wa sumu nyingi na mafuta mengi mwilini hasa katika mishipa na ogani za uzazi
- Kutokufanya mazoezi
- Matumizi ya pombe kali, na uvutaji wa sigara
- Uzito mkubwa (uliopindukia, uliokithiri), na Kitambi
- Kutokukaa sawa kwa vichocheo vya mwili (Hormone Imbalance)
- Maambukizi ya Magonjwa ya zinaa(kama gonorrhea na chlamydia)
-Maambukizi ya bakteria kutoka kwenye njia ya mkojo
- Kuumia kwa eneo la nyonga
- Kujizuia kukojoa mara kwa mara
- Umri mkubwa
- Upasuwaji wa korodani,matatizo ya kimaumbile ya Korodani
- Historia ya Familia (Kurithi) n.k.
DALILI ZA KUTANUKA KWA TEZI DUME
Tatizo la Tezi Dume si tatizo la kutokea tuu siku moja na mara moja tuu. Mpaka mtu apate saratani ya Tezi Dume (Prostate Cancer), atambue alianza kupata tatizo hilo kwa muda mrefu sana, Wengi wao hueleza dalili za tatizo hili huanza kuziona si chini ya miaka 3.
Hivyo ukiona dalili mojawapo kati ya hizi chukua tahadhari na hatua mapema kabla haijaharibu mfumo wako mzima wa uzazi ikiwa wewe ni mwanaume.
a) Dalili za awali
- Kukojoa mkojo uliochanganyikana na damu
- Kukojoa mkojo wenye mtiririko dhaifu
- Maumivu kwenye mfumo wa mkojo
- Kuhisi maumivu wakati wa kukojoa
- Kuhisi kibofu kimeja mkojo muda wote na ukienda kukojoa mkojo hautoki, lakini ukirudi kukaa unahisi kukojoa tena.
- Homa
- Kukojoa mara kwa mara wakati wa usiku
b) Dalili za mtu aliyeathirika zaidi na tatizo hili
- Kupata Maumivu ya mifupa hasa chini ya mgongo, kiuno na mbavu
- Miguu kuwa dhaifu
- Kushindwa kumudu tendo la ndoa, au Kuhisi maumivu makali wakati unamaliza tendo la ndoa
- Kushindwa kuzuia mkojo , pindi unapohisi kukojoa
- Kushindwa kuzuia haja kubwa
- Tumbo kujaa gesi mara kwa mara n.k.
• Soma: Tatizo la Mapunye Kichwani kwa Watoto wadogo
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
Reply
image quote pre code