Nigeria yadai DR Congo walitumia wachezaji wasiostahiki

Nigeria yadai DR Congo walitumia wachezaji wasiostahiki

#1

Nigeria yadai DR Congo walitumia wachezaji wasiostahiki kwenye mechi ya kufuzu Kombe la Dunia

Nigeria inataka Fifa kuangalia ustahiki wa baadhi ya wachezaji waliochezeshwa na DR Congo katika fainali ya kombe la dunia la Afrika 2026.Chanzo cha picha,Getty Images

Maelezo ya picha,Nigeria inataka Fifa kuangalia ustahiki wa baadhi ya wachezaji waliochezeshwa na DR Congo katika fainali ya kombe la dunia la Afrika 2026.

Nigeria inatarajia kuongeza nafasi yake ya kufuzu Kombe la Dunia mwaka ujao baada ya kuwasilisha malalamiko FIFA, ikidai kuwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DR Congo) ilitumia wachezaji wasiostahiki kwenye fainali ya kufuzu ya Afrika mwezi uliopita.

DR Congo ilishinda dhidi ya Super Eagles kwa penalti na kupata nafasi ya kucheza mechi ya kufuzu mashindano ya kimataifa Machi, ambayo itatenga nafasi mbili za mwisho za Kombe la Dunia katika Canada, Mexico na Marekani.

Madai ya Nigeria kuhusu “udanganyifu” yanahusu wachezaji waliobadilisha taifa lao la kimataifa hivi karibuni na kujiunga na timu pinzani.

Shirikisho la Soka la Nigeria (NFF) linaamini wachezaji kama Aaron Wan-Bissaka na Axel Tuanzebe, ambao walicheza mchezo huo Morocco, hawakuwa na sifa za kucheza kwani sheria za Kongo haziruhusu uraia pacha.

Shirikisho la Soka la Kongo (Fecofa) limekataa malalamiko hayo. “Suala letu ni kwamba FIFA ilidanganywa na kuwaruhusu kucheza,” alisema katibu mkuu wa NFF, Mohammed Sanusi. “Sheria za Kongo haziwaruhusu kuwa na uraia wa pacha, lakini baadhi ya wachezaji wao wana pasipoti za Ulaya na Ufaransa. Hii ni kinyume cha kanuni za FIFA. Tunadai ilikuwa ni udanganyifu.”

NFF imesema tayari imewasilisha nyaraka na hoja za kisheria kwa FIFA.

BBC imewasiliana na FIFA kwa maoni na inasubiri majibu.

Fecofa, kwa upande wake, imedai malalamiko hayo ni jaribio la “kushinda mlango wa nyuma.” “Kombe la Dunia lazima lichezwe kwa heshima na kujiamini, si kwa ujanja wa mawakili,” ilisema chapisho kwenye mitandao rasmi ya Leopards.

Ujumbe huo pia uliwataja Wana-Nigeria kama “washindwa mbaya” na kutupilia mbali malalamiko hayo kama mwenendo mbaya wa michezo.

Changia Mada hapa(Reply)


image quote pre code