Mjasiriamali na bilionea wa teknolojia Elon Musk ameandika historia mpya baada ya kuwa mtu wa kwanza duniani kufikia utajiri wa dola za Marekani bilioni 600 sawa na Quadrilion 1.4, kulingana na takwimu za Forbes.
Hatua hiyo imechangiwa kwa kiasi kikubwa na kampuni yake ya anga, SpaceX, ambayo imezindua mpango wa kuuza hisa unaothamini kampuni hiyo kufikia dola bilioni 800 ongezeko kubwa kutoka dola bilioni 400 zilizokuwepo mwezi Agosti.
Musk, ambaye anamiliki takriban asilimia 42 ya SpaceX, amenufaika moja kwa moja na ongezeko hilo la thamani. Utajiri wake umeongezeka kwa dola bilioni 168, na kufikia takriban dola bilioni 677 kufikia siku ya jana Jumatatu.
Kwa mafanikio haya, Musk anakuwa mtu wa kwanza katika historia ya dunia kufikia kiwango hicho cha utajiri. Kulingana na rekodi za Forbes, hakuna mtu mwingine aliyewahi kufikia hata dola bilioni 500 hapo awali.









image quote pre code