Tatizo la kunuka mdomo,tatizo la mdomo kutoa harufu,chanzo na Tiba

Tatizo la kunuka mdomo, tatizo la mdomo kutoa harufu,chanzo na Tiba Shida hii ya kutoa harufu mbaya kinywani huwasumbua watu wengi, na wengine hushtuka baada ya kuambiwa kwamba Wakati wanaongea kuna harufu mbaya inatoka mdomoni, Katika makala hii tumechambua zaidi kuhusu chanzo cha tatizo la kutoa harufu mbaya mdomoni pamoja na Dawa nzuri ya kutoa harufu mbaya mdomoni. Chanzo cha tatizo la kutoa harufu mbaya mdomoni Tatizo hili husababishwa na nini? zipo sababu mbali mbali ambazo huchangia kinywa kutoa harufu mbaya, BAADHI YA SABABU HIZO NI PAMOJA NA; - Baadhi ya vyakula, baada ya chakula kuvunjwa vunjwa na baadhi ya mabaki ya chakula kuganda kuzunguka meno huweza kupelekea mashambulizi ya bacteria pamoja na kinywa kuanza kutoa harufu mbaya, Kula VITUNGUU MAJI, vitunguu saumu(garlic) au viungo vingine huweza kuongeza harufu mdomoni - Uvutaji wa Sigara ikiwemo Tumbaku, mbali na kuwa kwenye hatari ya kupata magonjwa ya fizi(gum disease) na meno,wavutaji wa sigara ikiwemo tumbuku wapo kwe...