Safari za Lagos zainyanyua Air Tanzania Kimataifa

Safari za Lagos zainyanyua Air Tanzania Kimataifa

#1

Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL) @airtanzania_atcl imepata utambuzi wa kimataifa kutoka Serikali ya India, siku chache baada ya kutangaza safari mpya ya moja kwa moja kati ya Dar es salaam na Lagos, Nigeria ambapo utambuzi huo umekuja kutokana na uendeshaji wake wenye uwazi, uadilifu na kufuata viwango vya juu vya kitaifa na kimataifa.



Safari hizo za Lagos zinatarajiwa kuanza Agosti 2025 ikiwa na lengo la kukuza biashara na kuimarisha ushirikiano kati ya Afrika Mashariki na Magharibi, ikiwa ni sehemu ya mkakati wa ATCL wa kupanua huduma za kimataifa na kuiweka Tanzania kwenye ramani ya anga barani Afrika.

Kwa mujibu wa Bodi Kuu ya Kodi za Ndani na Forodha ya India (CBIC) ATCL ni miongoni mwa kampuni chache barani Afrika zinazofuata viwango vinavyotakiwa katika sekta ya anga ambapo Meneja Uhusiano wa Kampuni hiyo Sarah Reuben amesema, “Tunajivunia kutambuliwa na Serikali ya India. Hii ni ishara kuwa Air Tanzania iko tayari kushindana kimataifa kwa ubora wa huduma.”

Aidha Safari ya Lagos inafuatia uzinduzi wa safari ya Kinshasa (DRC) mwezi Aprili 2025, hatua zinazodhihirisha dhamira ya kampuni hiyo kuboresha usafiri wa anga barani Afrika.

Related Discussions

REPLY HAPA


image quote pre code