CHANZO CHA GESI TUMBONI

CHANZO CHA GESI TUMBONI

#1

Kukiwa na hitilafu katika uzalishwaji wake kunaweza kuzalishwa kwa wingi zaidi na kiasi huweza kubadilika na kuwa katika mfumo wa hewa (gesi) ambayo hujaa tumboni na kuweza kupanda hadi kwenye njia ya juu ya chakula na kufika kooni.

Kwa hiyo, kiungulia na tumbo kujaa gesi hutokana na matatizo katika uzalishwaji na ufanyaji kazi wa asidi hii ya tumboni mwetu.

Hivi ni baadhi ya vitu ambavyo vinaweza kusababisha au kuongeza uzalishwaji wa asidi nyingi tumboni na kuweza kupelekea au kuongeza matatizo ya kiungulia na tumbo kujaa gesi.

Maambukizi ya bakteria wajulikanao kama Helicobacter pylori ambao husababisha vidonda vya tumbo

Saratani (Kansa) kwenye tumbo au utumbo

Kula chakula kingi

Baadhi ya vyakula na viungo kama vile vyakula vya mafuta mengi, vyakula vilivyokaangwa, nyanya, vitunguu, matunda jamii ya machungwa/machenza, vitunguu swaumu nk

Maziwa na bidhaa zitokanazo na maziwa

Kafeini (Kama kwenye kahawa, soda, chai nk)

Msongo

Uvutaji wa sigarakiungulia 1

Pombe

Uzito mkubwa na uzito uliopitiliza

Tiba:

Cha msingi sana ni kujua kitu gani kinasababisha tatizo hilo kwako na kisha kuanza kuacha na kukiepuka kabisa.

Kama ni magonjwa basi kwanza yadhibitiwe vizuri ili asidi isizidi kuzalishwa zaidi, kama ni vyakula na vinywaji basi ni vyema kuviepuka.

Kuna dawa nzuri kabisa zipo ambazo ni mahususi kwa ajili ya kupunguza uzalishwaji wa asidi hiyo au kupunguza asidi ambayo tayari imeshazalishwa. Hivyo ni vyema kuonana na wataalaum wa Afya kwa msaada zaidi



Related Discussions

REPLY HAPA


image quote pre code