UTI
• • • • • •
DALILI ZA UTI KWA WAJAWAZITO
Dalili za UTI zimegawanywa katika makundi matatu.
1) UTI ambayo haina dalili (asymptomatic UTI)
2) UTI inayohusisha kibofu(cystitis) na njia ya mkojo(urethritis) na kwa ujumla wake inaitwa kitaalamu kama Lower UTI
3) UTI inayohusisha njia ya mkojo itoayo mkojo kwenye figo(ureteritis) na figo (nephritis na sio kidneytis) pamoja na pyelonephritis hizi kwa ujumla hufahamika kitaalam kama Upper UTI.
1) UTI ambayo haina dalili (asymptomatic UTI)
Kama jina hili linavojioeleza ni kwamba watu hawa hawatajijijua kama wana UTI na hawatakua na dalili yeyote ile ya maambukizi. Watu hawa wanakua na kiasi kidogo cha vimelea ambao hawatoshi kumletea mtu shida yeyote.
Mara nyingi hawa watu hugundulika kwa Bahati mbaya tu na ni pale mkojo ukipimwa kama sehem ya uchunguzi ndipo unagudua kumbe kuna vimelea kadhaa kwenye mkojo.Mara nyingi hii haihitaji tiba Bali hata kunywa maji mengi pia inatisha kabisa kuondoa hicho kias kidogo cha vimelea.
2) UTI inayohusisha kibofu(cystitis) na njia ya mkojo(urethritis) na kwa ujumla wake inaitwa kitaalamu kama Lower UTI
Sasa hapa ndipo mtu huanza kupata vidalili vya hapa na pale na dalili kuu za UTI iliyoshambulia maeneo haya ni:-
1) Kupata maumivu wakati wa kukojoa(dysuria)
2) Kupata hisia za mkojo kua wa moto sana wakati wa kukojoa(burning sensation)
3) kukojoa Mara kwa Mara(urinary frequency)
4) Kuhisi kukojoa kila SAA hats kama huna mkojo(urgency)
5) Kupata maumivu,mkereketo kwenye tumbo chini ya kitovu na juu ya sehemu ziotapo nywele za siri(suprapubic pain).
6) Homa(fever),ukipima joto hua juu ya 37.5 centigrade.
7) Kuhisi baridi sana na kutetemeka tetemeka(rigors and chills)
Kw ushauri zaidi,elimu au Tiba tuwasiliane kwa namba +255758286584.
REPLY HAPA
image quote pre code