Halafu wanataka tena twende Zanzibar tukacheze mchezo wa fainali-Mtine
Mtendaji Mkuu wa Klabu ya Yanga Andre Mtine baada ya kutoka Ofisi za TFF ameendelea kusisitiza msimamo wao kama klabu ni kulipwa fedha za zawadi ya bingwa wa Kombe la CRDB Federation ambalo Yanga ndio bingwa kwa misimu mitatu mfululizo iliyopita.
Mtine amesema, duniani kote bingwa anapaswa kupewa zawadi zake na sio kukatwa kwa ajili ya kulipa madeni au mambo mengine.
Siku mbili zilizopita tuliwaandikia [TFF] kwa maandishi na kuwapa msimamo wetu.
“Halafu wanataka tena twende Zanzibar tukacheze mchezo wa fainali, tulipie usafiri, bonus kama tutashinda ubingwa. Tunamudu vipi hizo gharama?—————amehoji Mtine.
REPLY HAPA
image quote pre code