UTE
• • • • • •
UTE UNAOASHIRIA SIKU YA KUPATA UJAUZITO
.
ningependa kuzungumzia swala la ute wa uzazi kwa undani zaidi ili kila mmoja wetu aelewe ni vipi ute huu unaonekana na lini unaonekana. Fuatilia
Kwa kawaida hormone zinazochochea mayai kutengenezwa ndo hizo hizo zinachochea kutengenezwa kwa ute unaosaidia mbegu za kiume zijongee vizuri.
Hormone ya estrogen ndo inahusika na hili. Endapo una estrogen kidogo huwez pata ute au kama mfumo wa estrogen na progesterone haujakaa katika uwiano mzuri huwezi pata ute.
Ute unaovutika huanza kutokea siku chache kabla ya yai kuachiliwa.
Japo wengine wenye tatizo la Polycystic ovarian syndrome wanakua wanapata ute huu zaidi ya mara moja katika mizunguko yao.
Ute huu unapozalishwa unaambatana na joto kupanda. Kama unapata ute na joto hakuna ni mabadiliko na inaweza kua haupevushi mayai
JINSI YA KUANGALIA UTE
1. nawa mikono na ufute iwe mikavu
2. weka kidole cha kati ukeni ndani. Kama unatoa ute mwingi basi haina haja ya kuingia ndani
3. toa kidole na kuangalia ute ukoje
AINA ZA UTE
1.MKAVU /DRY PHASE
Uke siku zote hauwi mkavu kabisa, Unapokuwa katika kipindi hiki unakua tu na majimaji kiasi na hayavutiki wala kunata.
Ute huu uanza kutokea ndani ya Siku 1 hadi 3 tokea umalize period.
2.STICKY
Siku ya nne hadi 6 baada ya kumaliza hedhi unaanza kutengeneza ute unaokua unanata kama gundi fulani. Ute huu unapokuwepo hauwezi kupata mimba kwani unaathiri kujongea vizuri kwa mbegu za kiume.
3.CREAMY
Ndani ya siku ya 7 hadi 9 Unaanza kutengeneza ute ambao unakua mithili ya lotion na haunati.
Kipindi hiki ndio mwili unakua unajiandaa kuingia katika hali ya hatari. kwa watu wanotafuta watoto basi anaweza kuanza kushiriki tendo la ndoa kwa ajili ya kutafuta mtoto.
4.EGGY WHITE
Kuanzia siku ya 10 hadi 15 hapa ukeni unakuwa na ute unaovutika uko mithili ya ute wa yai bichi kama inavyo onekana pichani hapo chini. Unapopata ute huu ni dalili kwamba upo katika siku za hatari na yai limepevuka.
Baada ya siku za hatari unarudia tena kupata ute ulio kama lotion(creamy) hadi utapofikia hedhi ya mwezi unaofatia.
REPLY HAPA
image quote pre code