KONGOSHO
• • • • •
CHANZO CHA TATIZO LA KUVIMBA KWA KONGOSHO,dalili na Tiba (pancreatitis)
Pancreatitis, Hili ni Tatizo la kutokea kwa uvimbe ndani ya kongosho,tatizo hili huonyesha dalili mbali mbali,
na katika makala hii tunachambua kuhusiana na sababu za tatizo hili,dalili, pamoja na tiba yake
CHANZO CHA TATIZO LA KUTOKEA KWA UVIMBE NDANI YA KONGOSHO
- Uvimbe ndani ya kongosho au kuvimba kwa kongosho husababishwa na Enzymes wa umeng'enyaji yaani DIGESTIVE ENZYMES,
ambao huanza kufanya kazi wakiwa bado ndani ya kongosho hali ambayo hupelekea kuvimba kwa seli ndani ya kongosho na hatimaye kuvimba kwa kongosho.
BAADHI YA SABABU AMBAZO HUONGEZA UWEZEKANO WA KUTOKEA KWA TATIZO HILI NI PAMOJA NA;
1. Mtu kuwa na kansa au Saratani ya kongosho
2. Tatizo la uzito kupita kiasi au Obesity
3. Mtu kuumia maeneo ya tumboni
4. Maambukizi ya vimelea mbali mbali vya magonjwa kama vile; Bacteria,Virusi pamoja na Fangasi
5. Uwepo wa kiwango kikubwa cha Calcium ndani ya damu
6. Uwepo wa kiwango kikubwa cha Triglyceride ndani ya damu
7. Mtu kuwa na tatizo la mawe kwenye kifuko cha nyongo yaani Gallstones
8. Matumizi ya baadhi ya dawa
9. Unywaji pombe kupita kiasi
10. Mtu kufanyiwa upasuaji wa tumbo
DALILI ZA TATIZO LA KUVIMBA KWA KONGOSHO
- Mtu kujisaidia kinyesi chenye harufu kama ya mafuta
- Uzito wa mwili kushuka kwa kasi
- Mtu kupata maumivu makali ya tumbo hasa akiliminya au kulishika
- Kupata hali ya kichefuchefu pamoja na kutapika
- Joto la mwili kupanda au mgonjwa kuwa na homa
- Maumivu ya tumbo upande wa juu
- Mtu kupata maumivu makali sana ya tumbo baada ya kula kitu chochote
- Mtu kupata maumivu ya tumbo ambayo husambaa hadi mgongoni
N.k
VIPIMO;
vipimo mbali mbali hufanyika kama vile; Ultrasound ya tumboni, Vipimo vya Damu(blood tests), Vipimo vya kinyesi(Stool tests) N.k
MATIBABU YA TATIZO HILI LA KUVIMBA KWA KONGOSHO
• Matibabu huhusisha njia mbali mbali kulingana na hali ya mgonjwa, na njia mojawapo ni;
Baada ya mgonjwa kufika hospital atakuwa chini ya uangalizi maalumu, huku akinyimwa kula kwa muda flani ili kongosho lirudi katika hali yake ya kawaida,
mgonjwa kuendelea kupata drips za maji yaani IV fluids, dawa za maumivu, Lakini pia kama itahitajika mgonjwa huweza kufanyiwa UPASUAJI.
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
REPLY HAPA
image quote pre code