Biden apokea ujumbe mwingi wa kumtia moyo baada ya kugundulika Saratani
Joe Biden ametoa shukrani baada ya kupokea msururu wa ujumbe wa kumtia moyo kutoka kote ulimwenguni, ikiwa ni pamoja na barua ya kibinafsi kutoka kwa Mfalme Charles wa Uingereza, baada ya rais huyo wa zamani wa Marekani kutangaza anaugua ugonjwa wa saratani siku ya Jumapili.
"Saratani inatugusa sote," Biden aliandika kwenye mtandao wa kijamii Jumatatu asubuhi. "Kama wengi wenu, Jill na mimi tumejifunza kwamba sisi ni wenye nguvu zaidi katika maeneo yaliyovunjika. Asante kwa kutuinua kwa upendo na msaada."
Siku ya Jumapili, ofisi ya Biden ilifichua kwamba aligunduliwa kuwa na aina kali ya saratani ya kibofu ambayo imeenea kwenye mifupa yake.
Taarifa hizo zinakuja huku maswali yakiibuliwa upya kuhusu afya ya rais huyo wa zamani alipokuwa madarakani.
Maelezo ya picha,Donald Trump na JD Vance wamehoji iwapo ukweli kuhusu afya ya Joe Biden ulifichwa wakati alipokuwa mamlakani
Rais Donald Trump alichapisha ujumbe wake akisema kwamba "amesikitika" kpokea taarifa kuhusu ugonjwa wa Biden lakini baadaye alihoji - bila kutoa ushahidi wowote - ikiwa timu ya Biden ilifahamu mapema kuhusu ugonjwa wake na kufahamisha umma kuhusu hali yake.
"Ninashangaa kuwa umma haukujulishwa muda mrefu uliopita kwasababu ya [saratani] kufika hatua ya tisa huchukua muda mrefu," alisema katika Ikulu ya White House Jumatatu alasiri.
"Inaweza kuchukua miaka kufikia kiwango hiki cha hatari," alisema, na kuongeza: "Ninahisi vibaya sana juu yake, na nadhani watu wanapaswa kujaribu kujua nini kilifanyika."
Ugunduzi wa kuchelewa wa saratani hata hivyo hutokea . Utafiti mmoja wa Uingereza mnamo 2014 uligundua 46% ya utambuzi wa saratani nchini humo ulifobainika katika hatua za juu.
Ofisi ya Biden ilisema kwamba aligunduliwa Ijumaa kuwa ana saratani ya kibofu "iliyoonyeshwa na alama ya Gleason ya 9 (Kikundi cha Daraja la 5) na kwenye mfupa".
"Wakati hii inaonyesha aina kali zaidi ya ugonjwa huo, saratani inaonekana kuwa kuwa na mwitikio wa homoni jambo ambalo linawezesha udhibiti mzuri."
Alama ya Gleason ya tisa inamaanisha ugonjwa wake umeainishwa kama "kiwango cha juu" na seli za saratani zinaweza kuenea haraka, kulingana na Utafiti wa Saratani nchini Uingereza.
Biden alisema uchunguzi wake ulifanywa baada ya kuripoti dalili za maambukizi ya njia ya mkojo ambazo zilisababisha madaktari kupata uvimbe mdogo ndogo kwenye kibofu chake.
Kufuatia utambuzi wa saratani, wengi wametoa kauli za kumtia moyo Biden akiwemo Rais wa zamani Barack Obama na Makamu wa Rais wa zamani Kamala Harris.
Mfalme Charles ameandika kwa faragha kwa Biden akitoa uungaji mkono wake na kumtakia mema, Buckingham Palace ilisema.
Mfalme, 76, ambaye amekutana na Biden mara kadhaa, pia anapokea matibabu ya aina isiyojulikana ya saratani baada ya saratani yake kugunduliwa mnamo 2024.
Biden alikuwa ametuma salamu zake za heri, akisema: "Nina wasiwasi naye. Nimesikia tu kuhusu ugonjwa wake. Nitakuwa nikizungumza naye, Mungu akipenda."
Maelezo ya picha,Ujumbe wa kumtia moyo Biden umemiminika kutoka kwa watu mbali mbali akiwemo Mfalme Chales wa Uingereza (pichani) , ambaye pia anaugua maradhi ya saratani isiyojulikana
Makamu wa Rais JD Vance alitoa salamu za heri, lakini alihoji ikiwa watu wa Amerika walikuwa na picha wazi ya afya ya Biden wakati rais wa zamani alipokuwa madarakani.
"Kwa kweli tunahitaji kuwa waaminifu kuhusu ikiwa rais wa zamani alikuwa na uwezo wa kufanya kazi," Vance alisema Jumatatu. "Na hilo ndilo... linaweza kutenganisha hamu yake ya kuwa na matokeo sahihi ya afya kwa kutambua kwamba iwe ni madaktari au kama kulikuwa na wafanyakazi karibu na rais wa zamani, sidhani kama aliweza kufanya kazi nzuri kwa watu wa Marekani."
Vance pia alisema alilaumu watu walio karibu naye zaidi kuliko Biden mwenyewe.
"Huu sio mchezo wa watoto, na tunaweza kumuombea afya njema, lakini pia tutambue kuwa ikiwa huna afya ya kutosha kufanya kazi hiyo, hupaswi kufanya kazi hiyo," aliongeza.
Tangazo hilo linakuja huku Biden akijiepusha na ukosoaji kutoka kwa kitabu kinachokuja kinachodai yeye na washauri wake walificha ukweli kuhusu afya yake iliyokuwa ikidhoofika alipokuwa katika Ikulu ya White House.
Maelezo yaliyofichuliwa wiki iliyopita kutoka kwa kitabu kiitwacho, Dhambi ya Asili: Kuzorota kwa Rais Biden, Kufunika Kwake, na Chaguo Lake baya la kuwania tena mamlaka , ni pamoja na Biden kutomtambua muigizaji na mfadhili wa mara kwa mara wa chama cha Democratic, George Clooney katika uchangishaji fedha mwaka jana na wasaidizi wakijadili kumuweka rais huyo wa zamani kwenye kiti cha magurudumu.
Kitabu kitatolewa Jumanne.
Takriban mwaka mmoja uliopita, rais huyo wa zamani alilazimika kujiondoa katika uchaguzi wa rais wa Marekani wa 2024 kwasababu ya wasiwasi kuhusu afya yake na umri wake.
Via:Bbc
Reply
image quote pre code