Chanjo ya kwanza ya kisonono duniani yazinduliwa wakati maambukizi yakiongezeka
Uingereza itakuwa nchi ya kwanza duniani kuanza kutoa chanjo dhidi ya ugonjwa wa zinaa wa kisonono.
Haitapatikana kwa kila mtu. Lengo zaidi litakuwa kwa wanaume wenye kujihusisha na wapenzi wa jinsi moja na wapenzi wawili wenye historia ya kuwa na wapenzi wengi au waliokuwa na historia ya kupata magonjwa ya zinaa.
Chanjo hiyo ina ufanisi wa 30-40%, lakini NHS England inatumai kuwa itabadilisha idadi inayoongezeka ya maambukizi. Kulikuwa na kesi zaidi ya 85,000 mnamo 2023, ya juu zaidi tangu rekodi zilipoanza mnamo 1918.
Ugonjwa wa kisonono hauneshi dalili wakati wote, lakini zinaweza kujumuisha maumivu, kuvimba kwa sehemu za siri na utasa.
Ni watu wangapi watachagua kuchanjwa haijulikani. Lakini makadirio ya Chuo cha Imperial London yanaonesha kwamba ikiwa chanjo itathibitishwa kuwa maarufu basi inaweza kuzuia kesi 100,000
Max, mwanaharakati wa afya ya ngono, aliiambia BBC Newsbeat kuwa "100%" atachanja chanjo hiyo baada ya kugunduliwa na ugonjwa wa kisonono mara mbili ndani ya mwaka mmoja.
"Nadhani hii ni nzuri kwamba imetangazwa", anasema, na kuongeza: " ni ushindi mkubwa tu pande zote."
Chanjo itaanza kutolewa mwezi Agosti na itatolewa kupitia huduma za afya ya ngono.
Reply
image quote pre code