Profesa Janabi ashinda ukurugenzi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) kanda ya Afrika

Profesa Janabi ashinda ukurugenzi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) kanda ya Afrika

#1

Profesa Janabi ashinda ukurugenzi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) kanda ya Afrika

Mshauri wa Rais wa Tanzania Masuala ya Afya na Tiba ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Profesa Mohamed Yakub Janabi ametangazwa rasmi kushinda uchaguzi na amechaguliwa kwa kishindo kuwa Mkurugenzi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) kwenye uchaguzi uliofanyika leo May 18,2025 Geneva.

Uchaguzi huo umefanyika kuziba nafasi ambayo iliachwa wazi na aliyekuwa Mkurugenzi Mteule wa nafasi hiyo, Dkt. Faustine Ndugulile baada ya kufariki ambapo Prof Janabi alikuwa ni Mgombea pekee kutoka nchi za kusini mwa jangwa la Sahara, huku wenzake wanne wakitokea nchi za Afrika Magharibi akiwemo Dkt. N’da Konan Michel Yao (Ivory Coast), Dkt. Dramé Mohammed Lamine (Guinea), Dkt. Boureima Hama Sambo (Niger) na Prof. Mijiyawa Moustafa wa Togo.

Reply

image quote pre code