Pumu au Asthma ni nini? Fahamu hapa kila kitu

Pumu au Asthma ni nini? Fahamu hapa kila kitu

#1

Pumu au Asthma ni nini? Fahamu hapa kila kitu



Pumu ni ugonjwa wa kudumu wa mapafu unaowaathiri watu wa rika zote. Husababishwa na uvimbe na kubana kwa misuli ya njia za hewa, hali inayofanya kupumua kuwa vigumu.

Dalili ni kikohozi, kupumua kwa shida, na kubanwa kifua, dalili hizi zinabadilika kwa muda na kuongezeka wakati wa usiku au wakati wa mazoezi. Ingawa pumu inaweza kuwa hatari, inaweza kudhibitiwa kwa matibabu sahihi.

Athari za Pumu au Asthma ni nini?

Pumu mara nyingi haitambuliwi au haitibiwi ipasavyo, hasa katika nchi zenye kipato cha chini na cha kati.

Wanaoathirika wanaweza kukosa usingizi, kuwa na uchovu mwingi wa mwili,kushindwa kuconcentrate n.k.

Hii inaweza kuathiri masomo, kazi na kipato cha familia. Katika hali mbaya, mgonjwa huhitaji huduma ya dharura hospitalini na pumu kali inaweza kusababisha kifo.

Dalili za Pumu au Asthma ni nini?

Kwa mujibu wa shirika la afya Duniani(WHO) dalili za pumu zinaweza kutofautiana, zikiwa mbaya zaidi usiku au wakati wa mazoezi. Dalili hizo ni pamoja na

• Kikohozi kinachoendelea, hasa usiku
• Kupata shida wakati wa kupumua
• Kupumua kwa shida hata ukiwa umepumzika
• Kubanwa kifua n.k.

Vichochezi vikuu ni kama vumbi, moshi, poleni, manyoya, sabuni zenye harufu kali na manukato.

Chanzo cha pumu ni nini?

Vitu hivi huongeza hatari ya Mtu kupata Pumu

• Historia ya pumu katika familia hususani kutoka kwa wazazi
• Magonjwa mengine ya mzio au allergy kama eczema na mafua ya mzio
• Kuishi mijini
• Uzito mdogo au kuzaliwa njiti, moshi wa tumbaku na maambukizi ya virusi
• Vichochezi vya mazingira kama uchafuzi wa hewa, vumbi na kemikali
• Uzito kupita kiasi au utipwatipwa



Matibabu ya Pumu au Asthma ni nini?

Hakuna tiba ya kuponya kabisa pumu, lakini kuna matibabu ya kudhibiti. Dawa kuu hutolewa kwa kuvutwa kupitia kifaa maalum au inhaler 

• Vifaa kama Bronchodilators mfano salbutamol hufungua njia za hewa

• Steroids mfano beclometasone hupunguza uvimbe na hatari ya mashambulizi makali ya pumu

Baadhi ya wagonjwa huhitaji kutumia inhaler kila siku. Kutumia spacer hufanya inhaler kuwa rahisi zaidi, hasa kwa watoto.

Spacer inaweza kutengenezwa kwa chupa ya plastiki. Upatikanaji wa inhaler ni changamoto katika baadhi ya nchi hasa masikini.

Huduma binafsi

Wagonjwa na familia zao wanahitaji elimu kuhusu pumu, jinsi ya kuepuka vichochezi na kutumia mpango wa matibabu. Kufahamu lini inapaswa kuongeza matibabu ni muhimu ili kuepuka mashambulizi makali ya pumu.

Mambo muhimu kuhusu ugonjwa wa pumu

Pumu ni ugonjwa usioambukiza  au (NCD), unaowaathiri watoto na watu wazima, na ndiyo ugonjwa wa muda mrefu wa kawaida zaidi kwa watoto

Uvimbe na kubanwa kwa njia ndogo za hewa kwenye mapafu husababisha dalili za pumu, ambazo zinaweza kuwa mchanganyiko wowote wa kikohozi, kubanwa na kifua, kupumua kwa shida, na kufurukuta.

Pumu iliwaathiri watu takriban milioni 262 mwaka 2019 na ulisababisha vifo 455,000.

Dawa za kuvuta au (inhaler) zinaweza kudhibiti dalili za pumu na kuwawezesha watu wenye pumu kuishi maisha ya kawaida na kushiriki shughuli mbalimbali.

Kuepuka vichochezi vya pumu pia kunaweza kusaidia kupunguza dalili za pumu.

Vifo vingi vinavyohusiana na ugonjwa wa pumu hutokea katika nchi zenye kipato cha chini na cha kati, ambako tatizo la kutogunduliwa na kutotibiwa ipasavyo ni changamoto.

Kwa mujibu wa WHO,wao wamejikita kuboresha utambuzi, matibabu na ufuatiliaji wa pumu ili kupunguza mzigo wa kimataifa wa magonjwa yasiyoambukiza na kupiga hatua kuelekea huduma za afya kwa wote

Reply


image quote pre code