TANZIA:Charles Hillary, Mtangazaji nguli wa zamani wa BBC afariki dunia

TANZIA:Charles Hillary, Mtangazaji nguli wa zamani wa BBC afariki dunia

#1

TANZIA:Charles Hillary, Mtangazaji nguli wa zamani wa BBC afariki dunia



Mtangazaji wa zamani wa BBC Idhaa ya Kiswahili, Charles Hilary ameafariki dunia alfajiri ya leo Jumapili, Ikulu ya Rais Zanzibar imetangaza.

Hilary ambaye amejizolea umaarufu Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla kwa kazi yake ya utangazaji amefikwa na umauti akiwa ni Mkurugenzi wa idara ya mawasiliano Ikulu ya Zanzibar na msemaji mkuu wa serikali ya Zanzibar.

Taarifa ya Ikulu inaeleza kuwa kifo chake kimetokea katika hospitali ya Mloganzila jijini Dar Es Salaam. Taarifa kutoka kwenye familia inaeleza kuwa alikimbizwa katika hospitali hiyo baada ya kuugua ghafla akiwa nyumbani kwake.

Hilary alijiunga na BBC mwaka 2006 na kuwa sehemu muhimu ya timu ya watangazaji wa habari na pia kipindi cha Ulimwengu wa Soka kinachorusha matangazo ya mpira wa Ligi Kuu ya England kila wikendi.

Alikuwa pia sehemu ya watangazaji wa awali wa matangazo ya televisheni ya Dira TV mwaka 2012. Mwaka 2015 aliondoka BBC baada ya kuhudumu kwa miaka tisa na kurejea nyumbani Tanzania.

Safari yake ya utangazaji ilianza mwanzoni mwa miaka ya 1980 akiwa na Radio Tanzania Dar Es Salaam (RTD) sasa TBC na akaibuka kuwa moja ya sauti za dhahabu katika matangazo mubashara ya mpira wa miguu wa zama zake.

Mwaka 1994 alikuwa moja ya watangazaji waandamizi walioanzisha stesheni ya Radio One Sterio jijini Dar Es Salaam na akiwa hapo akapata jina lake maarufu la ‘Mzee wa Charanga’ kutokana na umaarufu wa kipindi cha muziki wa charanga ambacho alikuwa akitangaza.

Aliondoka Rario One na kujiunga na Idhaa ya Kiswahili ya DW nchini Ujerumani mwaka 2003, na alijiunga na BBC akitokea huko.

Aliporudi Tanzania alijiunga na Azam TV mwaka 2015 mpaka alipoteuliwa kuwa msemaji wa Ikulu ya Zanzibar mwaka 2021.

Reply


image quote pre code