Waziri Mkuu mstaafu Cleopa Msuya afariki dunia

Waziri Mkuu mstaafu Cleopa Msuya afariki dunia

#1

Waziri Mkuu mstaafu Cleopa Msuya afariki dunia



Dar es Salaam. Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ametangaza kifo cha aliyewahi kuwa Makamu wa kwanza wa Rais na Waziri Mkuu, Cleopa Msuya kilichotokea saa 3 asubuhi ya leo Jumatano, Mei 7, 2025 katika Hospitali ya Mzena, Kijitonyama jijini Dar es Salaam.

Akitangaza msiba huo kwa Taifa, Rais Samia amesema Mzee Msuya ameugua tatizo la moyo kwa kipindi kirefu na kupata matibabu ndani ya nchi katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete, Mzena na nje ya nchi huko London nchini Uingereza.

“Natoa pole kwa familia, ndugu, jamaa na marafiki kwa msiba huu mkubwa kwa Taifa na natangaza siku saba za maombolezo kuanzia tarehe 7 hadi 13 (Mei) ambapo bendera zitapepea nusu mlingoti,” amesema Rais Samia.

Amesema taarifa zaidi kuhusu msiba huo zitaendelea kutolewa na Serikali.

Mzee Msuya amefikwa na umauti akiwa na miaka 94. Alizaliwa Januari 4, 1931 katika Kijiji cha Chomvu Usangi, Wilaya ya Mwanga, Mkoa wa Kilimanjaro.

Reply


image quote pre code