Mama mzazi wa Msanii Hawa Hussen maarufu Carina amefariki dunia
Mama mzazi wa Msanii Hawa Hussen maarufu Carina aitwaye Fatma Maruzuku amefariki dunia leo June 06,2025 ikiwa haijapita hata miezi miwili tangu tangu alipofariki Mwanae Carina.
Kaka wa Marehemu Mama Carina amethibitisha kifo hicho ambapo amesema alikuwa anaugua na presha na kisukari na hakuweza hata kushiriki arobaini ya Mtoto wake wiki iliyopita.
Mama Carina atazikwa katika makaburi ya Kisutu kesho June 07,2025 saa 10 jioni.
Itakumbukwa Mwigizaji Hawa Hussein Ibrahim ( Carina) alizikwa April 19,2025 katika Makaburi ya kisutu Dar es salaam baada ya kufariki India alipokuwa akipatiwa matibabu kutokana na matatizo ya tumbo yaliyokuwa yana msumbua.
REPLY HAPA
image quote pre code