Kutokwa na damu wakati wa haja kubwa chanzo na Tiba

Kutokwa na damu wakati wa haja kubwa chanzo na Tiba

#1

Kutokwa na damu wakati wa haja kubwa chanzo na Tiba

Kutokwa na damu wakati wa haja kubwa (rectal bleeding) kunaweza kusababishwa na mambo mbalimbali, kutoka matatizo madogo hadi makubwa zaidi. Hapa chini ni vyanzo vya kawaida na maelezo ya kila kimoja 

1.Ugonjwa wa bawasiri (Hemorrhoids)

Bawasiri huhusisha mishipa ya damu kuvimba kwenye sehemu ya haja kubwa (rectum au anus).

Dalili mojawapo ni: Damu wakati wa kujisaidia au Vitone vya damu baada ya kujisaidia.

Kula vyakula vyenye nyuzinyuzi, kunywa maji mengi, epuka kukaa muda mrefu chooni, na kutumia krimu maalum (kwa ushauri wa daktari).

2. Kupata michubuko au majeraha kwenye tundu la haja kubwa (Anal fissure)

Kwa Sababu mbali mbali ikiwemo ya kupata choo kigumu

Dalili: Maumivu makali wakati au baada ya kujisaidia, damu kama matone n.k.

3. Maambukizi kwenye utumbo (Infection / Colitis)

Maambukizi kutoka kwa bakteria (kama Shigella, E. coli), virusi au vimelea kama amiba (amoeba). huweza kusababisha dalili kama hizi: 

  • Kuharisha damu, 
  • tumbo kuuma, 
  • homa.n.k.

4. Vidonda vya utumbo mpana (Ulcerative colitis)

Dalili kama hizi huweza kutokea: Kuharisha damu, maumivu ya tumbo, kupungua uzito.n.k...

 5. Saratani ya utumbo mpana (Colon cancer / polyps)

Vinyama (polyps),uvimbe,au Saratani unaweza kusababisha damu kwenye haja.

6. Sababu nyingine ni pamoja na:

  • Kutumia dawa zinazoweza kusababisha taizo la damu kutokuganda (anticoagulants), 
  • vidonda vya tumbo, 
  • au mzio wa chakula.n.k..

Nini cha kufanya:

Nenda hospitali ukiona: 

-Damu inatoka mara kwa mara.

-Damu ni nyingi sana

-Una maumivu makali, homa au kupungua uzito.

-Epuka kujitibu bila uchunguzi.n.k...

KWA USHAURI ZAIDI NA TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Changia Mada hapa(Reply)


image quote pre code