UK yaidhinisha wagonjwa mahututi kupewa Msaada wa kujitoa Uhai

UK yaidhinisha wagonjwa mahututi kupewa Msaada wa kujitoa Uhai

#1

Wabunge wa Uingereza wameuidhinisha muswada wa sheria ya kuwaruhusu wagonjwa mahututi na ambao ni watu wazima kupewa msaada wa kumaliza uhai wao.



Baada ya miezi kadhaa ya majadiliano makali, muswada huo umefanikiwa kuvuuka kihunzi cha kwanza hivi leo kabla ya kuidhinishwa rasmi kuwa sheria miezi michache inayokuja.

Mnamo mwezi Novemba mwaka uliopita wabunge walio wengi waliunga mkono pendekezo la kuandaliwa muswada wa sheria ya kuruhusu huduma ya msaada wa kifo kwa kura 330, huku waliopinga wakipata kura 275.

Chini ya mapendekezo ya muswada huo, wagonjwa wenye akili timamu walio na umri kuanzia miaka 18 lakini walio kwenye hali mahututi na wanaokadiriwa kuwa na muda usiozidi miezi sita ya kuishi wataweza kuomba huduma ya kukatisha uhai wao katika miji ya England na Wales. Na ili kutimiza hilo, mgonjwa mahututi atatakiwa kuwa na uwezo wa kumeza mwenyewe dawa zitakazokatisha maisha yake.

REPLY HAPA


image quote pre code