WHO: Jinsi ya kusaidia afya ya akili katika nyakati za misukosuko

WHO: Jinsi ya kusaidia afya ya akili katika nyakati za misukosuko

#1

Mwongozo wa WHO: Jinsi ya kusaidia afya ya akili katika nyakati za misukosuko



Zaidi ya watu milioni 300 duniani wanahitaji msaada wa kibinadamu kutokana na migogoro, mabadiliko ya tabianchi, misukosuko ya kisiasa na majanga ya asili. Na hali hiyo imeongeza uhitaji mkubwa wa huduma za afya ya akili na msaada wa kisaikolojia limesema shirika la Umoja wa Mataifa la afya ulimwenguni WHO.

Ili kukabiliana na changamoto hiyo, WHO kwa kushirikiana na mashirika mengine ya Umoja wa Mataifa ambayo ni lile la masuala ya Watoto- UNICEF, linashughulikia masuala ya wakimbizi -UNHCR, la idadi ya watu na afya ya uzazi - UNFPA na wadau wengine, wameunda Mfumo wa Huduma za Msingi za Afya ya Akili na Msaada wa Kisaikolojia (MSP).

Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Magonjwa yasiyoambukiza na Afya ya Akili wa WHO Dévora Kestel amesema mfumo huu unatoa mwongozo wa haraka kuhusu nini kifanyike kwenye dharura ili kuhakikisha msaada unawafikia walioathirika kwa wakati. “Katika majanga, maamuzi yanapaswa kufanywa haraka na fedha kutengwa ili hatua za kipaumbele zichukuliwe. MSP inatoa mwongozo wa kuratibu shughuli muhimu na kuhakikisha msaada unafika kwa walengwa,” amesema,

Mfumo huu umeundwa kwa kuzingatia uzoefu wa kimataifa na unajumuisha nyenzo  kuu saba:

Mwongozo wa MSP wa huduma za msingi.

Mafunzo ya MSP.

Miongozo ya haraka ya sekta mbalimbali.

Viashiria vya kutumika wakati wa ufuatiliaji na tathmini (M&E)

Zana za tathmini ya mahitaji kwa sekta nyingi.

Hifadhidata ya ripoti za tathmini na ramani.

Hifadhidata ya mafunzo ya MHPSS.

Kwa mujibu wa WHO, mwongozo huu mpya unasaidia sekta tofauti kupanga na kushirikiana, kuhakikisha msaada wa afya ya akili na kisaikolojia unakuwa wa haraka, bora na unaojali mahitaji ya jamii zilizoathirika.

Changia Mada hapa(Reply)


image quote pre code