karibu watu 300 wamekufa kutokana na janga la mafuriko Pakistan
Waokoaji nchini Pakistan wameipata miili zaidi ya watu waliofukiwa kwenye vifusi vya majengo yaliyoporomoka kutokana na mafuriko makubwa yaliyoikumba wilaya moja kaskazini magharibi mwa nchi hiyo.
Hadi sasa karibu watu 300 wamekufa kutokana na janga hilo lililotokea katika wilaya ya Buner.
Wakaazi wa vijiji vya wilaya hiyo wanasema watu wengine kadhaa bado hawajapatikana na juhudi za kuwatafuta zimeelekezwa kwenye vifusi vya majengo yaliyoanguka kutokana na maji mengi ya mafuriko yaliyotitirika kutoka maeneo ya milima.
Mafuriko hayo yamesababishwa na mvua kubwa za masika ambazo pia zimeleta maafa ikiwemo vifo katika jimbo linalozozaniwa baina ya India na Pakistan la Kashmir.
image quote pre code