Utafiti mpya Unywaji wa pombe na kuongezeka kwa hatari ya saratani ya kongosho

Utafiti mpya Unywaji wa pombe na kuongezeka kwa hatari ya saratani ya kongosho

#1

Utafiti mpya Unywaji wa pombe na kuongezeka kwa hatari ya saratani ya kongosho



Muungano mkubwa wa kimataifa wa tafiti unaoongozwa na watafiti kutoka Shirika la Kimataifa la Utafiti juu ya Saratani (IARC) ambalo ni shirika tanzu la Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani, WHO na taasisi wadau, wamechunguza uhusiano kati ya unywaji wa pombe na hatari ya kupata saratani ya kongosho.

Taarifa iliyochapishwa leo Mei 26 jijini Lyon, France inafafanua kwa matokeo, yaliyochapishwa katika jarida la PLOS Medicine, yanaonesha uhusiano mdogo lakini muhimu kati ya matumizi ya pombe na hatari ya saratani ya kongosho, bila kuathiriwa na jinsia au hali ya uvutaji sigara.

Tathmini hiyo ilikusanya data kutoka kwa vikundi 30 vya watu waliokusanywa kutoka mabara manne (Asia, Australia, Ulaya, na Amerika Kaskazini). Vikundi hivyo vilihusisha takriban watu milioni 2.5 ambao hawakuwa na saratani mwanzoni mwa utafiti, waliosajiliwa kati ya mwaka 1980 na 2013 wakiwa na wastani wa umri wa miaka 57. Katika kipindi cha wastani cha ufuatiliaji wa miaka 16, kesi 10,067 za saratani ya kongosho ziliripotiwa.

“Unywaji wa pombe unajulikana kuwa sababu ya kusababisha saratani, lakini hadi sasa ushahidi wa kuhusiana kwake moja kwa moja na saratani ya kongosho umekuwa haueleweki vyema,” anasema Dkt. Pietro Ferrari, Mkuu wa Kitengo cha Lishe na Kimetaboliki katika IARC na mwandishi mkuu wa utafiti huo. “Matokeo yetu yanatoa ushahidi mpya kuwa saratani ya kongosho huenda ikawa aina nyingine ya saratani inayohusiana na matumizi ya pombe, uhusiano ambao umeonekana kupuuzwa hadi sasa.”

Matokeo muhimu

Tafiti za awali za matarajio zimependekeza kuwa pombe inaweza kuwa na athari mbaya katika kusababisha saratani ya kongosho, hasa pale matumizi yanapozidi gramu 30 za ethanoli kwa siku (g/siku), sawa na karibu vinywaji viwili vya kawaida vya pombe kwa siku.

Katika utafiti huu mpya, ilibainika kuwa kila ongezeko la 10 g/siku katika matumizi ya pombe lilihusishwa na ongezeko la asilimia 3 ya hatari ya kupata saratani ya kongosho.

Kwa kina zaidi, kwa wanawake, ikilinganishwa na unywaji wa pombe wa 0.1–5 g/siku (matumizi madogo), matumizi ya 15–30 g/siku yanahusishwa na ongezeko la asilimia 12 ya hatari ya saratani ya kongosho. Kwa wanaume, ikilinganishwa na unywaji wa pombe wa 0.1–5 g/siku, matumizi ya 30–60 g/siku yanahusishwa na ongezeko la asilimia 15, huku matumizi ya zaidi ya 60 g/siku yakihusishwa na ongezeko la asilimia 36 ya hatari ya saratani hiyo.

“Pombe mara nyingi hutumiwa pamoja na tumbaku, jambo ambalo limezua maswali kuhusu ikiwa uvutaji sigara unaweza kuchanganya uhusiano huu,” anaongeza Dkt. Ferrari. “Hata hivyo, uchambuzi wetu ulionesha kuwa uhusiano kati ya pombe na hatari ya saratani ya kongosho uliendelea kuonekana hata kwa watu wasiovuta sigara, ikimaanisha kuwa unywaji wa pombe peke yake ni sababu huru ya hatari ya kupata saratani ya kongosho.”

Saratani ya Kongosho: Tatizo linalokua kiwango cha kimataifa

Saratani ya kongosho imeibuka kuwa changamoto kubwa ya afya ya umma katika miaka ya hivi karibuni. Ingawa ni aina ya 12 ya saratani kwa uwingi duniani, mwaka 2022 ilichangia karibu asilimia 5 ya vifo vyote vinavyohusiana na saratani duniani, kutokana na kugunduliwa kwa kuchelewa na kiwango kikubwa cha vifo.

Viwango vya kuugua na kufariki kutokana na saratani ya kongosho barani Ulaya, Amerika Kaskazini, Australia na New Zealand, na Asia ya Mashariki ni mara 4–5 zaidi ya maeneo mengine. Licha ya maendeleo katika matibabu ya saratani, bado kuna mafanikio machache katika kuokoa maisha ya waathiriwa wa saratani ya kongosho.

“Ingawa kuna sababu kadhaa zinazojulikana kama vile matumizi ya tumbaku, unene wa kupindukia, uvimbe sugu wa kongosho, na kisukari, sababu za saratani ya kongosho bado hazieleweki vyema. Utafiti huu unatoa uelewa mpya kuhusu nafasi ya unywaji wa pombe katika mwanzo wa saratani ya kongosho,” anasema Dkt. Ferrari. “Utafiti zaidi unahitajika ili kuelewa vyema nafasi ya matumizi ya pombe katika maisha yote, kwa mfano wakati wa ujana, na athari za mifumo mahususi ya matumizi kama vile unywaji wa pombe kupita kiasi kwa mara moja (binge drinking).”

Reply


image quote pre code