Elimu zaidi kuhusu Saratani ya Matiti itolewe kwa umma

Elimu zaidi kuhusu Saratani ya Matiti itolewe kwa umma

#1

Elimu zaidi kuhusu Saratani ya Matiti itolewe kwa umma.



Mkurugenzi msaidizi wa huduma za Mama na mtoto wa Wizara ya Afya Dkt. Felix Bundala amezitaka taasisi za umma pamoja na mashirika binafsi kuungana kwa pamoja ili kutoa elimu kuhusu saratani ya matiti kwa jamii ili kushinda mapambano dhidi ya ugonjwa huo. 

Dkt. Bundala ameyasema hayo  Mei 7, 2025 jijini Dodoma wakati akizindua awamu ya pili ya ya Mradi wa Huduma za Saratani ya Matiti Uchunguzi Mpaka Tiba unaodhaminiwa na Taasisi ya Pfizer kwa kushirikiana na Jhpiego, na kutaka elimu zaidi itolewe kwa jamii ili kukabiliana na ugonjwa huo.

“Tumekutana hapa sio kwa ajili ya kuweka mikakati ya kupambana na saratani ya matiti bali kuona namna ya kupunguza mahangaiko kwa muhusika na pia kwa jamii kwa ujumla, tunafaamu kuwa sio wote wanohudhuria kwenye vituo vya kutolea huduma wanakutwa na tatizo ndio maana tunatakiwa kutoa elimu ya kutosha kwa watoa huduma ili waweze kutoa huduma ipasavyo kwa yeyote anayefika kwenye kituo cha kutolea huduma ya saratani,” amesema Dkt. Bundala.

Aidha Dkt. Bundala amesema matibabu ya  ugonjwa wa saratani ya matiti yana gharama ya moja kwa moja na isiyo ya moja kwa moja ikiwemo msongo wa mawazo kwa mgonjwa na jamii inayomzunguka pia.

“Matibabu ya ugonjwa huu ni ghali sio tu kwa namna tunavyokabiliana na mwanamke anayesumbuliwa na saratani ya matiti bali hata gharama anazotumia zile zisizo za moja kwa moja na zile za moja kwa moja,” amesema Dkt. Bundala.

Dkt. Bundala ameiomba taasisi ya Pfizer kupanua wigo ili kuwafikia watu wengi zaidi kwaajili kutoa huduma hiyo inayohitajika katika mapambano dhidi ya Saratani ya matiti.

“Sasa tunakwenda katika awamu ya pili ambapo kutakuwa na watoa huduma 45 vituo vya kutolea huduma 124 katika mikoa minne ninashukuru sana kwa nia hii njema ya kuongeza wigo lakini pia kuanza katika  mikoa mingine mipya ambayo itahitaji uwekezaji mkubwa li kusaidia watu wengi zaidi. Tunavyo jiandaa kwaajili ya kupanua wigo wa huduma hii tunatakiwa kuangalia namna ya kutumia rasilimali zilizopo ili kufikia malengo ya mkakati huu ambao ni kuishinda saratani ya matiti,” amesema Dkt. Bundala.

Awamu ya kwanza ya mradi huu ilianza mwaka 2024 na kutoa huduma katika mikoa ya Tanga, Mwanza na Visiwani Zanzibar ambapo watu 28,053 walichunguzwa, lakini kwa awamu hii ya pili mwaka 2025 mikoa miwili imeongezeka na kufanya idadi ya mikoa kufikia minne na Tanzania visiwani na itaendelea hadi mwaka 2027, ikiwalenga wanawake wenye umri wa miaka 30 hadi 50 pamoja na wanaume.

Reply


image quote pre code