Breaking:Mwigulu nchemba waziri Mkuu wa Tanzania

Breaking:Mwigulu nchemba waziri Mkuu wa Tanzania

#1

Mwigulu nchemba waziri Mkuu wa Tanzania

Mbunge wa Iramba Magharibi Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba ameteuliwa kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ambapo endapo atathibitishwa na Wabunge atahudumu kama Waziri Mkuu wa 12 wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Mussa Azzan Zungu, ametangaza jana kuwa Leo tarehe 13 Novemba 2025, Bunge la 13 katika Mkutano wa Kwanza, Kikao cha Tatu, litakuwa na shughuli muhimu ya kuthibitisha uteuzi wa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, sambamba na uchaguzi na uapisho wa Naibu Spika wa Bunge.

Zungu ametoa kauli hiyo leo, tarehe 12 Novemba 2025, wakati akiahirisha kikao cha pili cha Bunge, Jijini Dodoma. Amesisitiza kuwa ni muhimu kwa wabunge wote kuhudhuria kikao hicho bila kukosa, kutokana na uzito wa ajenda zilizopangwa kujadiliwa.

Ikumbukwe kuwa Bunge hili la 13 lilianza Jumanne, tarehe 11 Novemba 2025, likianza na uchaguzi wa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kisha kiapo cha uaminifu na ahadi ya uzalendo kwa wabunge wateule, zoezi ambalo limehitimishwa siku ya jana.

Kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 (kama ilivyorekebishwa), uteuzi wa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hufanyika kwa kufuata utaratibu maalum unaoanza mara baada ya Rais kuapishwa rasmi kushika madaraka.

Ibara ya 51(1) ya Katiba, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ndiye mwenye mamlaka ya kumteua Waziri Mkuu, ambapo mteule lazima awe Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Katiba inaeleza kuwa uteuzi huo unapaswa kufanyika ndani ya siku kumi na nne (14) tangu Rais kuapishwa, na mteule anatakiwa kuwa Mbunge kutoka chama chenye wabunge wengi zaidi bungeni, au ikiwa hakuna chama chenye wingi, basi awe Mbunge anayekubalika na wabunge wengi.

Baada ya uteuzi huo, jina la Waziri Mkuu mteule hupelekwa Bungeni kwa ajili ya kuthibitishwa kupitia Azimio la Bunge litakaloungwa mkono na kura nyingi za wabunge waliohudhuria kikao. Mteule atathibitishwa rasmi endapo atapata uungwaji mkono wa wabunge wengi.

Mara baada ya kuthibitishwa, Waziri Mkuu hula kiapo cha uaminifu na ahadi ya uadilifu mbele ya Rais au mtu aliyeidhinishwa naye, ndipo huanza rasmi kutekeleza majukumu yake.

Kwa mujibu wa Ibara ya 52 ya Katiba, Waziri Mkuu ndiye Kiongozi wa Shughuli za Serikali Bungeni na husimamia utekelezaji wa sera na shughuli za Serikali ya Muungano kwa niaba ya Rais.

Mwigulu Lameck Nchemba ni nani?

Mwigulu Lameck Nchemba Madelu ni mwanasiasa Mtanzania na mwanachama wa chama cha kisiasa cha CCM ambaye amekuwa waziri wa fedha na mipango tangu 31 Machi 2021.

Mwigulu Nchemba

Alisoma uchumi kwenye Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam alipohitimu shahada ya uzamili kwenye mwaka 2006.

Amechaguliwa kuwa mbunge wa Iramba Magharibi mwaka 2010 akarudishwa bungeni kwa miaka 2015 – 2020. Mwaka 2015 alikuwa naibu waziri ya fedha. Baada ya uchaguzi wa 2015 aliteuliwa kuwa waziri wa kilimo, ila mwaka 2016 alibadilishwa kuwa waziri wa mambo ya ndani.

Mwaka 2018 aliondolewa katika nafasi hiyo na rais John Magufuli aliyetaja kasoro katika wizara yake kama vile ulaji rushwa, matumizi mabaya ya fedha na kuongezeka kwa ajali barabarani ilhali mhusika haonekani[1]. Rais alitaja mkataba wa Lugumi ambako polisi ilipata hasara ya Tsh bilioni 30, kashfa ya mkataba kwa vifaa vibovu kwenye idara ya NIDA, uigizaji wa magari na malori 700 kwa polisi, mkataba usio halali kwa sare za polisi. Pamoja na hayo watazamaji wengine waliuliza kama jinsi Nchemba alivyojaribu kutafuta mapatano na kanisa la KKKT baada ya barua ya maaskofu ya Pasaka 2018 ilijenga wasiwasi wa rais dhidi yake [2].

Katika Februari 2019 Nchemba aliumia katika ajali ambako gari lake liligonga pundamilia wawili barabarani[3]

Tarehe 2 Mei 2020 aliteuliwa kuwa waziri wa Sheria na Katiba baada ya kifo cha waziri Augustine Philip Mahiga.[4]

HistorySource:Wikipedia

Changia Mada hapa(Reply)


image quote pre code