Ticker

6/recent/ticker-posts

Madhara na namna ya kutibu tatizo la kupinda nyayo kwa watoto



 Madhara na namna ya kutibu tatizo la kupinda nyayo kwa watoto

Nyayo kupinda ni tatizo linaloweza kumfanya mtoto kushindwa kucheza na wenzake na kushindwa kufanya vizuri darasani.Matibabu ya mapema yatamsaidia mtoto kuwa katika hali nzuri kisaikolojia, kifikira, masomo na hata kuchangamana vizuri na wenzake katika michezo.

⚠️Je wajua,tatizo hili la kupinda nyayo za miguu (feet pronation) linaweza kumsababishia mtoto wako kupata ulemavu wa kudumu endapo lisipo tibiwa mapema?

▪️Tatizo hili la kupinda nyayo za miguu [Feet Pronation] na kukosa uvungu [Flat feet/Pes Planus/Webbed Feet] ni tatizo linalo weza kutibika pasipo kufanyiwa upasuaji (Surgery/Operation ) na pia bila dawa ya aina yeyote.

▪️Tatizo hili linaweza kutibika kwa vifaa tiba saidizi { Supramalleolar Orthoses -SMO na Arch support insoles} ambavyo hutumiwa kwa kipindi cha kuanzia miezi sita,tisa hadi miezi 12 na kupona kabisa endapo mtumiaji atavitumia kwa muda wote na kwa usahihi zaidi.

?Madhara ya tatizo hili la kupinda miguu na kukosa uvungu ni makubwa hasa mtoto anapozidi kukua,kuongezeka uzito na kukomaa mifupa yake ,kama vile;
▪️Kupinda kwa nyayo za miguu (feet pronation) na nyayo kukosa uvungu(flat feet/Pes planus) ambayo itamfanya muonekano wake wa mwili kutokuwa sawa(bad morphology )
▪️Kupata maumivu makali kwenye maungio mbalimbali kama vile kwenye enka (Ankle joint pains),magoti (knee joint pains),nyonga (hip joint pains) pamoja na maumivu ya mgongo (Cervical-lumber pain) ambayo yata msababishia kushindwa kutembea umbali mrefu kwa kutumia miguu yake.

▪️Tatizo hili pia linaweza kumfanya mtoto ashindwe kujiamini hasa anapo vaa viatu na hupelekea viatu kupinda ndani ya muda mfupi na kuwa kama na miguu ya bata (flat feet) na kumfanya ashindwe kushiriki shughuli mbalimbali za kiu-kakamavu (heavy duty exercises like running,sports activities and parading ).

▪️Tatizo hili linaweza kumsababishia pia wakati mwingine mgongo kutengeneza umbile la “S” kwa maana ya kibyongo kutokana na kutokuwa na uwiano Sawa wa uzito wa mwili (unequal body weight line due to foot mis-alignment).

?Tafadhali mpendwa mchunguze leo mtoto wako ,ikiwa ana hilo tatizo umlete apate suluhisho mapema akiwa bado vifupa yake haijakomaa kwani bado anaweza kukaa sawa kabisa.