Ticker

6/recent/ticker-posts

Je ni afya Kunywa Maji wakati wa kula au baada ya kula?



 Je ni afya Kunywa Maji wakati wa kula au baada ya kula?

Kumekuwa na maneno mengi sana kwenye jamii zetu huku kila mmoja akiamini chake,

Wengine wanasema huruhusiwi kunywa maji na chakula,wengine wanasema unatakiwa kukaa baada ya nusu saa baada ya kula ndyo unywe maji,

pamoja na maneno mengine mengi,je kipi ni sahihi?

UKWELI NI KWAMBA;

Hakuna ushahidi wowote wa kisayansi kwamba ukinywa maji wakati unakula chakula huweza kuvuruga mpangilio wa umeng'enyaji chakula,

Na zaidi ya hapo,kunywa maji wakati au baada ya chakula husaidia sana kwenye umeng'enyaji wa chakula,

maji pamoja na vimiminika vingine kama juice huweza kusaidia kuvunja vunja chakula na kuurahisishia mwili kufyonza virutubisho au Nutrients,

Maji pia husaidia kulainisha haja kubwa na kusaidia kuzuia tatizo la kujisaidia choo kigumu yaani constipation

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA JUU YA TATIZO LOLOTE TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.