Airtel sasa kutumia Intaneti ya Musk Afrika

Airtel sasa kutumia Intaneti ya Musk Afrika

#1

Airtel sasa kutumia Intaneti ya Musk Afrika



DUBAI — Kampuni ya Airtel Africa imetangaza leo makubaliano na SpaceX, inayomilikiwa na Elon Musk, kuleta huduma ya Starlink — intaneti ya kasi kubwa kupitia setilaiti — kwa wateja wake barani Afrika. Hii ni baada ya mafanikio yaliyopatikana nchini India.

Kwa sasa, SpaceX imepata leseni za kuendesha huduma katika nchi 9 kati ya 14 ambazo Airtel Africa inaendesha shughuli zake, huku leseni kwa nchi nyingine 5 zikiwa bado katika mchakato.

Kupitia ushirikiano huu, Airtel Africa itaweza kuongeza upatikanaji wa intaneti katika maeneo ya mbali, mashule, vituo vya afya na kwa biashara mbalimbali. Pia wataangazia kupanua mtandao wa simu vijijini kwa kutumia teknolojia ya cellular backhaul ya Starlink.

Airtel na SpaceX pia wamekubaliana kuendelea kuchunguza maeneo mengine ya ushirikiano ili kuongeza ushirikishwaji wa kidijitali barani Afrika, huku SpaceX ikinufaika na miundombinu ya ardhini ya Airtel barani humo.

#HabariLEOUPDATES

Reply


image quote pre code