Ticker

6/recent/ticker-posts

SHINGO YA MTOTO KULEGEA(CHANZO CHAKE)



 SHINGO YA MTOTO KULEGEA(CHANZO CHAKE)

Mabadiliko ya Watoto wengi huanza kwenye miezi mitatu ya Mwanzo wakati ambapo Shingo ya mtoto huanza kuimarika na kuwa na nguvu ya kutosha ili kuweza kuinua na kusupport kichwa chake.

Uwezo huu wa shingo huimarika kabsa na kuwa na nguvu inayotakiwa kuweza kusupport kichwa cha mtoto(full control) kwenye miezi sita ya Mwanzo.

KUMBUKA; Sio lazima iwe hivo kwa kila mtoto, kuna baadhi ya watoto shingo inakuwa imekaza toka mwanzoni, na wengine huchelewa zaidi kujenga misuli Imara shingoni na kuifanya iwe STABLE.

Ili kujua kwamba baada ya mtoto kuzaliwa misuli yake ya shingoni(neck muscles) sio imara na haina nguvu,utaona akijaribu kuinua kichwa chake kinashuka chenyewe,

Hii ina maana misuli hii ya shingoni sio imara na haina nguvu ya kuweza kusupport kichwa chake.

Hivo basi katika kipindi hiki utatakiwa kumsupport mtoto kichwa chake pamoja na shingo yake kwa kutumia mikono yako.

MWEZI MMOJA MPAKA MIEZI MIWILI

- Kwa baadhi ya watoto mwishoni mwa mwezi wa Kwanza,wanaanza kujaribu kuinua kichwa, na pia wanaweza kupeleka kichwa kidogo upande mmoja kabla ya kichwa kurudi kilipokuwa.

WIKI NNE MPAKA WIKI 12

- Mpaka kufikia kipindi cha Wiki 12, Kwa baadhi ya watoto wanakuwa tayari wana uwezo wa kuinua kichwa vizuri bila shida yoyote.

NB: Uwezo wa mtoto kwenye ukuaji wake huweza kuwa tofauti na mwingine(Babies develop skills differently), Baadhi ya watoto huwahi zaidi kwenye hatua hizi na wengine huchelewa zaidi.

Lakini kama Mtoto wako anazaidi ya Miezi 5 mpaka 6 bado shingo haina dalili yoyote ya kukaza na hawezi kudhibiti kichwa chake vizuri unaweza kuongea na wataalam wa afya kwa ajili ya ushauri zaidi.

FAHAMU: Kama mtoto wako kazaliwa kabla ya Wiki 37 za Ujauzito anaweza kupata shida hii ya shingo kuchelewa kukaza pamoja na kuchelewa kwenye hatua zingine za ukuaji wake(development milestones).

Hapa nazungumzia hatua kama vile;

• Mtoto kuanza Kukaaa

• Mtoto kutambaa

• Mtoto kusimama

• Mtoto kutembea

• Mtoto kuongea n.k

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA JUU YA TATIZO LOLOTE TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.