CHANZO CHA GESI TUMBONI KWA MTOTO ANAYENYONYA
fahamu baadhi ya sababu ambazo huweza kusababisha tatizo la Gesi tumboni kwa mtoto wako anayenyonya, je wajua tatizo la gesi tumboni huweza kusababisha mtoto kulia lia kila mara? soma makala hii kufahamu vyanzo mbali mbali vya tatizo hili la gesi tumboni kwa mtoto wako anayenyonya.
1.Mtoto kunyonya wakati chuchu ya mama anayenyonyesha haijafunika vizuri mdomo wa mtoto, hali hii hupelekea mtoto kunyonya maziwa pamoja na hewa wakati wa unyonyeshaji,
Mama anayenyonyesha hushauriwa kuhakikisha chuchu imefunika mdomo wa mtoto vizuri hasa ile sehemu nyeusi ya ziwa, ili kuhakikisha mtoto hanyonyi hewa wakati wa unyonyeshaji
2. Maziwa ya mama kutoka kwa kasi sana, maziwa ya mama yanapotoka kwa kasi sana husababisha mtoto kunyonya harakaharaka na kupelekea mtoto kumeza hewa nyingi,
Unashauriwa kukamua kidogo ziwa ili kupunguza kasi ya utokaji wa maziwa kabla ya kumnyonyesha mtoto wako
3. Mtoto kupaliwa sana,ambapo kwa asilimia kubwa hutokana na mtoto kutokupakatwa vizuri wakati wa unyonyeshaji pamoja na maziwa kutoka kwa kasi sana,Hali hii huweza kupelekea tatizo la gesi kujaa tumboni kwa mtoto
4. Mtoto mwenyewe kunyonya kwa harakaharaka,hii huweza kutokea wakati mtoto akiwa na njaa sana au maziwa kutoka kwa kasi na mtoto kushindwa kuyamudu
5. Umri wa mtoto,watoto wachanga hawana uwezo wa kumudu hewa inayoingia kwenye mfumo wa chakula,hivyo kadri mtoto anavyokuwa mdogo ndivo uwezekano wa kusumbuliwa na tatizo la Gesi tumboni huongezeka,
Unashauriwa kumbeulisha mtoto mara kwa mara na usisubiri tu mpaka amalize kunyonya kama wakina mama wengi walivyozoea
6. Aina ya maziwa anayopewa mtoto,Kwa watoto wanaotumia maziwa mbadala ya watoto wachanga,wanaweza kusumbuliwa sana na tatizo la gesi tumboni sababu ya aina ya maziwa wanayopewa pamoja na utumiaji wa chupa za chuchu kwa watoto,Credit:@via JJbreastfeedingstore.
KUMBUKA; Maziwa ya mama ni bora zaidi kuliko maziwa ya aina yoyote ile kwa mtoto wako,hivo kama kuna uwezekano wa mtoto kupata maziwa ya mama pekee,hakikisha anapata kwa kipindi chote cha angalau miaka miwili(2).
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA JUU YA TATIZO LOLOTE LILE TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.