KANISA la TAG kujenga hospitali za kisasa 32 nchi nzima

KANISA la TAG kujenga hospitali za kisasa 32 nchi nzima

#1

MOROGORO; KANISA la Tanzania Assemblies of God (TAG) limeanzisha mpango mkakati na endelevu wa kujenga hospitali za kisasa 32 mikoani ikiwa ni sehemu ya kuungana na serikali katika kuhakikisha huduma bora za afya zinawafikia kwa karibu wananchi wote.



Makamu Askofu Mkuu wa TAG, Dk Magnus Mhiche alisema hayo hivi karibuni eneo la Mkundi, Manispaa ya Morogoro wakati wa uzinduzi wa eneo la uwanja patakapojengwa Hospitali ya Uzima ikiwa ni mojawapo ya hospitali 32 zinazotarajiwa kujengwa nchini.

Alisema kwa sasa utaratibu unaendelea kufanyika kwa kushirikiana na wadau wakiwemo wahisani wa kanisa ili kupata gharama halisi zitakazotumika katika ujenzi wa hospitali hizo 32 kwa maana ya moja kwa kila mkoa Tanzania Bara pamoja na upande wa Zanzibar.

Askofu Mhiche alisema kujengwa kwa Hospitali ya Uzima mkoani Morogoro na katika eneo la Mkundi, Manispaa ya Morogoro itachangia utoaji na upatikanaji wa huduma bora za afya kwa wananchi.

“Huu ni mradi mkubwa unaogharimu milioni ya fedha na utakapokamilika utawanufaisha wana Morogoro na Watanzania wengi,” alisema Mhiche.

Alieleza kuwa ujenzi wa hospitali mkoani Morogoro inatarajiwa wakati wowote mwaka huu na utakamilishwa mwakani na kwamba kanisa linatarajia ifikapo mwaka 2033 hospitali zote zitakuwa zimekamilika na kufanya kazi.

Naye Katibu Mkuu wa Kanisa la Bethel Revival Temple (BRT), Dk Christopher Magomba alisema kukamilika kwa ujenzi wa hospitali hizo nchini, kutaonesha nia ya dhati ya Kanisa la TAG kuungana na serikali kuendelea kuboresha utoaji wa huduma ya afya.

Kwa upande wake, Mwakilishi wa Mganga Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dk Johanes Rwenyagila alilipongeza Kanisa la TAG kwa azma ya kujenga Hospitali ya Uzima na itakapokamilika itaongeza idadi ya hosiitali za umma na taasisi binafsi kufikia 25 ndani ya mkoa huo.

Related Discussions

REPLY HAPA


image quote pre code