Trump amuonya Musk kuwa atarudi kwao Afrika Kusini

Trump amuonya Musk kuwa atarudi kwao Afrika Kusini

#1

Rais wa Marekani Donald Trump ametishia kusitisha mabilioni ya dola ya ruzuku zinazotolewa kwa kampuni za Tesla na SpaceX zinazomilikiwa na bilionea Elon Musk kufuatia mvutano unaoendelea kati yao ambapo hii ni baada ya Musk kukosoa vikali mswada mpya wa kodi na matumizi ya Serikali unaolenga kufuta ruzuku za ununuzi wa magari ya umeme hatua inayotajwa kuathiri moja kwa moja kampuni ya Tesla.



Trump amenukuliwa akisema kuwa bila ruzuku hizo, Musk atahitaji kufunga biashara na kurudi nyumbani Afrika Kusini, kauli iliyozua mjadala mpana nchini humo na kwa upande wake, Musk hakusita kujibu kwa maneno makali akisema, “Zuia kila kitu sasa.”

Aidha mabishano haya yameibuka wakati ambapo Seneti ya Marekani imepitisha mswada huo kwa kura chache tu huku soko la hisa la Tesla likiripotiwa kushuka kwa asilimia kubwa ambayo ni ishara ya wasiwasi kwa wawekezaji kuhusu mustakabali wa kampuni hiyo.

@dw_kiswahili

Related Discussions

REPLY HAPA


image quote pre code