Atolewa Mbavu ili kuwa na Kiuno Chembamba Zaidi
Mitandao ya kijamii imetikiswa siku kadhaa nyuma baada ya mwanadada Emily James, msanii wa mitandaoni (influencer) kutoka Marekani, kufichua kuwa amefanyiwa upasuaji wa kipekee kwa kuondolewa mbavu sita (tatu kila upande) ili apate kiuno chembamba zaidi.
Emily alidai kwa ujasiri kuwa yeye ndiye wa kwanza duniani kuondoa mbavu zote, jambo lililoibua gumzo kubwa na mjadala mkali mtandaoni. Wengi walilaani hatua hiyo wakisema inaweza kupelekea matatizo makubwa ya kiafya kwa wanawake wanaohangaika kubadilisha maumbile yao ili kufikia kile kinachoitwa umbo bora.
Upasuaji huo uliripotiwa kumgharimu takribani dola 17,000 (zaidi ya shilingi milioni 40 za Kitanzania). Licha ya lawama na ukosoaji, Emily alisisitiza kuwa huo ni mwili wake na ana uhuru wa kufanya anachotaka, akifichua pia kuwa anapanga kuzitumia mbavu hizo kutengeneza taji (crown).
Tukio hili limechochea mazungumzo mapana kuhusu viwango vya urembo, mitazamo ya miili, na hatua ambazo baadhi ya watu wako tayari kuchukua ili kufuata mitindo ya mwonekano wa kuvutia.
image quote pre code