Madhara ya typhoid,fahamu hapa kila kitu
Yapo Madhara mbali mbali ya Ugonjwa wa typhoid
Ugonjwa wa typhoid au homa ya matumbo kama haujatibiwa unaweza kusababisha madhara makubwa mwilini mwako na wakati mwingine hata kifo
Moja ya madhara yake ni pamoja na:
(i)Kuvuja damu kwa ndani(Internal bleeding).
(ii)Kutoboka kwa utumbo:Intestinal perforation (a hole in your intestines).
(iii)Kuvimba au kupasuka kwa kifuko cha nyongo(Swollen or burst gallbladder).
(iv)Kupata matatizo kwenye Ubongo kama kuchanganyikiwa:Neurological (brain) symptoms, including confusion, delirium and seizures.
(v)Kuvimba eneo la kuzunguka Ubongo:Swelling around your brain (meningitis).
(vi)Tatizo kwenye mfumo wa hewa;Bronchitis, pneumonia or other respiratory issues.
(vii)Kupata maambukizi kwenye mifupa:Bone inflammation (osteomyelitis).
(viii) Moyo kuvimba:Heart inflammation.
(ix)Pamoja na matatizo mengine kama vile;figo kushindwa kufanya kazi(Kidney failure),Mimba kutoka zenyewe(Miscarriage).n.k.
Soma Zaidi hapa,Madhara hayo.........!!!!
Madhara ya typhoid
Madhara ya Typhoid (homa ya matumbo) hutokea pale ambapo ugonjwa haujatibiwa mapema au matibabu hayajakamilika. Baadhi ya madhara haya yanaweza kuwa ya muda mfupi au ya muda mrefu na mengine ni hatari kwa maisha.
Madhara ya kawaida na hatari ya typhoid ni pamoja na:
-
Kuvuja damu kwenye utumbo
- Kidonda hutoboa au kuharibu ukuta wa utumbo, na kusababisha kutokwa damu nyingi kwenye njia ya chakula.
- Dalili: kinyesi chenye damu au rangi ya mkaa, kuishiwa nguvu ghafla.
-
Kutoboka kwa utumbo (Intestinal perforation)
- Sehemu ya utumbo mdogo au mkubwa hutoboka, bakteria huenea tumboni na kusababisha maambukizi makubwa (peritonitis).
- Ni dharura ya upasuaji na inaweza kusababisha kifo haraka.
-
Maambukizi kuenea sehemu nyingine za mwili
- Maambukizi yanaweza kuenea kwenye moyo (endocarditis), mifupa (osteomyelitis), au mfumo wa mkojo.
-
Kuwashwa au kuvimba kwa ubongo (encephalopathy)
- Wagonjwa wachache hupata tatizo la kuchanganyikiwa, usingizi kupita kiasi, au kupoteza fahamu.
-
Uchovu sugu na kupungua uzito
- Hata baada ya kupona, baadhi ya watu hubaki na nguvu ndogo kwa wiki au miezi.
-
Kuwa mtoaji wa bakteria bila dalili
- Baada ya kupona, baadhi ya watu hubeba bakteria Salmonella typhi kwenye nyongo bila dalili na wanaweza kuwaambukiza wengine (carriers).
-
Vifo
- Bila matibabu sahihi, typhoid inaweza kuua hasa kwenye maeneo yenye huduma duni za afya.
Typhoid au Homa ya matumbo inaweza kuwa hatari ikiwa haitatibiwa haraka. Lakini kwa dawa za kisasa, watu wengi hupona kabisa. Kati ya mamilioni ya watu wanaogunduliwa na homa ya matumbo kila mwaka, takriban 1% hadi 2% ya visa ni hatari.
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
image quote pre code