Mtanzania akwama nchini Kenya kwa kudaiwa Fedha ya Matibabu milioni 120
Familia ya Harlequin Mlay ambaye ni Muongoza Watalii (Tour Guide) kutoka Tanzania, imewaomba Watanzania.. Ndugu, Jamaa na Marafiki pamoja na Serikali kutoa msaada wa mchango wa matibabu kwa ndugu yao huyo ambaye amepata matatizo ya kiafya akiwa nchini Kenya kwa shughuli za kikazi.
Familia imesema kuwa Harlequin Mlay akiwa Kenya alipatwa na hali ya dharura ya kiafya na kuwaishwa hospitalini akiwa hajitambui na baada ya vipimo Madaktari waligundua tatizo linalohitaji upasuaji wa kichwa ambao ulifanyika katika Hospitali ya Aga Khan, jijini Nairobi.
Kwa sasa, Mlay bado yuko katika Chumba cha ICU huku gharama za matibabu zikifikia shilingi milioni 120 za Kitanzania na zinaendelea kuongezeka na sasa Familia imelazimika kuja kwa Watanzania na Serikali kuomba michango ili kufanikisha malipo hayo ili Mlay aruhusiwe kuja nyumbani Nchini Tanzania kwa uangalizi zaidi wa kitabibu.








image quote pre code