Madhara ya bawasiri kwa mwanaume,Fahamu hapa

Madhara ya bawasiri kwa mwanaume,Fahamu hapa

#1

Madhara ya Bawasiri kwa Mwanaume ni yapi?

Bawasiri (pia huitwa hemorrhoids) ni uvimbe au mishipa ya damu iliyojaa kwenye eneo la haja kubwa au ndani ya puru. Ingawa huwapata watu wa jinsia zote, kwa wanaume inaweza kuleta changamoto kadhaa kiafya na kijamii ikiwa haitatibiwa mapema.

Aina za Bawasiri ni Zipi?

1. Bawasiri ya ndani (Internal hemorrhoids) – hupatikana ndani ya puru, mara nyingi haina maumivu lakini husababisha damu wakati wa haja kubwa.

2. Bawasiri ya nje (External hemorrhoids) – ipo nje ya puru, huweza kuuma sana na kuvimba. Hapa ndipo kinyama huonekana kujitokeza kwa nje....

Madhara ya Bawasiri kwa Mwanaume

1. Kutokwa na damu mara kwa mara

Wanaume wenye bawasiri hupoteza damu kidogo kila wanapojisaidia, hali ambayo huweza kusababisha upungufu wa damu (anemia) endapo itaendelea muda mrefu.

2. Maumivu na usumbufu wakati wa kukaa au kujisaidia

Hasa kwa wanaume wanaokaa muda mrefu (madereva, ofisini n.k.), bawasiri husababisha maumivu na kuchoma sehemu ya haja kubwa.

3. Kuvimba au kuonekana uvimbe nje ya puru

Hali hii husababisha kutojisikia vizuri na wakati mwingine kuchafuka kwa nguo kutokana na majimaji au uchafu unaotoka.

4. Kuwashwa au muwasho mkali sehemu ya haja kubwa

Hii hutokana na kuvuja damu au majimaji, na mara nyingine huleta maambukizi ya bakteria au fangasi.

5. Kupungua kwa hamu ya tendo la ndoa

Kwa sababu ya maumivu, wasiwasi, na msongo wa mawazo unaosababishwa na bawasiri.

  • Baadhi pia hata hamu ya tendo hupotea

6. Maambukizi (infection)

Endapo bawasiri itachanika, kuna hatari ya kupata maambukizi ya vimelea mbali mbali vya magonjwa ikiwemo:

  • Bacteria
  • Fangasi n.k.

7. Kupata matatizo ya haja kubwa 

Baadhi ya Wanaume hali hii ya Bawasiri huambatana na tatizo la kupata choo kigumu(constipation) au Wengine kushindwa kudhibiti haja kabsa.

Zingatia Tahadhari na Ushauri huu

-Epuka kukaa muda mrefu bila kusimama au kutembea.

-Kula vyakula vyenye nyuzi nyuzi (fiber) kama mboga, matunda, nafaka kamili.

-Kunywa maji mengi kila siku (angalau glasi 8–10).

-Epuka kunyanyua vitu vizito kupita kiasi.

-Usijizuie haja kubwa kwa muda mrefu— nenda chooni mara unaposikia haja.

-Ikiwa una damu au maumivu makali, muone daktari mapema kwa uchunguzi na matibabu sahihi.

AU KWA USHAURI ZAIDI,AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Changia Mada hapa(Reply)


image quote pre code