UGONJWA WA PID,VISABABISHI,DALILI ZA PID,MADHARA YAKE NA TIBA
➡️ Ombeni Mkumbwa
📶 SUMMARY: MAANA YA PID
Maambukizi Katika Mfumo wa Uzazi wa Mwanamke (PID)
Maambukizi katika mfumo wa uzazi wa mwanamke kwa kitaalamu Pelvic Inflamatory Diseases au kwa kifupi PID, ni moja ya matatizo ambayo huwaathiri sana wanawake. Kwa kawaida maambukizi haya huusisha shingo ya uzazi (cervix) hali ambayo hujulikana kama cervicitis, nyama ya mfuko wa uzazi (endometrium) ambayo kitaalamu huitwa endometritis, na mirija ya uzazi (fallopian tubes) hali ijulikanayo kitabibu kama salpingitis.
PID husababishwa na nini?
Pamoja na aina kadhaa za vimelea kuhusishwa na PID, vimelea vya jamii ya Neisseria Gonorrhoeae pamoja na Chlamydia trachomatis ndivyo vinavyoongoza kwa umaarufu zaidi katika kusababisha PID kwa akina mama.
Je mwanamke hupataje PID?
Kwa Njia hizi hapa chini ni rahsi sana kwa mwanamke kupata maambukizi katika via vyake vya Uzazi.
(1) Kufanya mapenzi au ngono isiyo salama
(2) Kupata maambukizi katika via vya uzazi mara baada ya mama tu Kujifungua ambapo kitaalam huitwa "POSTPARTUM INFECTION"
(3) Maambukizi ambayo mwanamke huweza kuyapata mara tu baada kutoa mimba kwa Njia zisizo salama kitaalam huitwa Post abortion infection au baada ya mimba kutoka yenyewe ambapo kitaalam huitwa post miscarrage infection
(4) Matumizi ya baadhi ya Njia za Uzazi wa mpango kama lupu au(IUCD) ambapo mwanamke kuweza kupata PID wakati wa uwekaji n.k
(5) Maambukizi kwa Njia ya damu kutoka kwa Mtu mwenye maambukizi katika via vya Uzazi
Dalili za PID ni zipi?
Zipo dalili kadhaa za ugonjwa huu wa PID. Miongoni mwa dalili hizi ni
Mwanamke kuhisi maumivu ya tumbo hasa maeneo ya chini ya kitovu
Kupata maumivu ya mgongo
Mwanamke kupata utoko mchafu sehemu za siri. Utoko huu huambatana na harufu mbaya.
Kuhisi maumivu wakati wa kukojoa
Kupata maumivu wakati wa tendo la ndoa
Kutoka damu bila mpangilio wakati wa hedhi
Kupata homa
Wakati fulani kuhisi kichefuchefu na
Pia kutapika
🔺MADHARA YA PID(MAAMBUKIZI KATIKA VIA VYA UZAZI VYA MWANAMKE)
Vipimo vya tatizo la PID
Baadhi ya vipimo kwa Mtu mwenye dalili za Ugonjwa wa PID ni kama ifuatavyo;
➖Kuchunguza mkojo kwenye darubini ili kutambua aina za vimelea vinavyomletea mgonjwa maambukizi. Lakini pia Mkojo huweza kutumiwa kwa kuoteshwa katika maabara kwa ajili ya kutambua aina nyingine za vimelea viletavyo maambukizi hayo.
➖Kipimo cha Damu kwa ajili ya kuchunguza vimelea mbali mbali vya Magonjwa ikiwemo PID,ambapo kitaalam kipimo hichi huitwa Full Blood Picture.
➖Uchanguzi wa utando unaozunguka shingo ya uzazi ambapo huweza kutumika vifaaa kama SPECULUM
➖Mwanamke mwenye dalili hizi kufanya kipimo cha ULTRASOUND
TIBA YA PID
Baada ya Ugonjwa wa PID kugundulika,mgonjwa atapewa dawa za kutibu ugonjwa huu. Shirika la Afya Duniani (WHO) limeonyesha baadhi ya miongozo na maelekezo ya kutibu Ugonjwa wa PID.
Baadhi ya dawa zilizoorodheshwa kwa ajili ya matibabu ya maambukizi katika via vya uzazi vya mwanamke(PID) ni pamoja na Cefotetan na Doxycycline; Clindamycin pamoja na Gentamycin; Ampicillin na Sulbactam kwa pamoja na Doxycycline; na Ceftriaxone au Cefoxitin pamoja na Doxycycline.
KINGA DHIDI YA UGONJWA WA PID
✓Kutokufanya ngono zembe kwani hiki ni mojawapo ya Chanzo cha Kupata ugonjwa wa PID
✓Kutokufanya tendo la ndoa mara tu baada Ya kujifungua kwani mlango wa uzazi utakuwa bado haujafunga vizuri na ni rahis kupata maambukizi pia
✓Fanya vipimo vya mara kwa mara hasa ukiwa na dalili kama nilizozitaja hapo juu
✓Muone mtaalam wa afya pale tu unapojihisi tofauti
NB: KAMA UNA TATIZO HILI NA MENGINE TUWASILIANE KUPITIA 0758286584 UKITUMA UJUMBE UTAJIBIWA KWA HARAKA ZAIDI.
#afyacheck_
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!