LIPS
• • • • •
CHANZO CHA TATIZO LA KUPASUKA MDOMO AU LIPS ZA MDOMO NA TIBA YAKE
Watu wengi hupatwa na tatizo la kupasuka Lips za mdomo na wengine kufikia hatua ya kuvuja damu kabsa mdomoni, Je tatizo hili hutokana na nini? na tiba yake ni nini?
CHANZO CHA TATIZO LA KUPASUKA LIPS ZA MDOMO
Kuna sababu zaidi ya moja ambayo huweza kuchangia uwepo wa tatizo hili, Na baadhi ya Sababu ambazo huongeza uwezekano wa mtu kupata shida hii ni pamoja na;
1. Mdomo kukauka au kuwa mkavu kwenye Lips kupita kawaida kutokana na sababu mbali mbali kama vile;
(i).Upungufu wa maji mwilini
(ii).Hali ya joto na jua kupita kawaida
(iii).Hali ya baridi kali
(iv).Upepo mkali,Hewa kavu(dry air) n.k
vyote hivi huweza kupelekea lips za mdomo kuwa kavu zaidi na kuchanika
2. Mtu kupata ajali au kuumia mdomoni pamoja na kwenye lips zake
3. Upungufu wa vitamins mwilini kama vile; Vitamin B ikiwemo, Niacin, Thiamine,folic acid n.k
4. Upungufu wa Madini mwilini kama vile madini chuma(Iron) na Zinc hupelekea lips za mdomo kupasuka hasa kwenye Corner ya mdomo
5. Lakini pia kukauka mdomo,lips kupasuka pamoja na vidonda mdomoni huweza kuwa dalili za homa ambazo hutokea wakati wa usiku n.k
6. Tatizo la Allergy au mzio
7. Lips za mdomo kuvimba hali ambayo hupelekea ngozi ya lips za mdomo kuvutika zaidi na kupasuka au kupata cracks.
MATIBABU YA TATIZO HILI
Kwa asilimia 100%, matibabu ya tatizo hili hutegemea na chanzo chake
- Epuka vitu vyote ambavyo huweza kusababisha tatizo hili kama vile kukaa kwenye jua sana n.k
- Kunywa maji ya kutosha, na kama una shida nyingine kama ya Allergy n.k ongea na wataalam wa afya kwa ajili ya matibabu zaidi
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
0 Comments