Dalili za Tetanus(pepopunda)baada ya mtu kuchomwa na kitu chenye Ncha kali
TETANUS
• • • • • •
Dalili za Tetanus(pepopunda) baada ya mtu kuchomwa na kitu chenye Ncha kali
Tetanus ni ugonjwa hatari sana ambao kwa kiswahili hujulikana kama Pepopunda,Ugonjwa huu huhusisha athari kwenye mfumo wa Fahamu inayosababishwa na sumu ya Bacteria(toxin-producing bacterium)
Sumu hii kutoka kwa Bacteria mtu huweza kuipata baada ya kuchomwa na vitu vya ncha kali kama vile Misumari,Mabati,Chupa,sindano n.k
DALILI ZA TETANUS AU PEPOPUNDA
-Wastani kutoka kuambukizwa hadi kuonekana kwa ishara na dalili (kipindi cha incubation) ni siku 10. Kipindi cha incubation kinaweza kuchukua siku 3 hadi 21.
Ishara na dalili za tetanus au pepopunda huanza pole pole kisha huendelea kuwa mbaya zaidi ndani ya wiki mbili. Kawaida dalili huanza kuonekana kwenye taya na kuendelea kushuka chini ya mwilini.
Ishara na dalili za pepopunda ni pamoja na:
1. Misuli ya mwili kuwa na maumivu makali na kuwa migumu au kukakamaa,ugumu wa misuli kwenye taya n.k
2. Mvutano wa misuli kuzunguka midomo yako, wakati mwingine hutengeneza kitu kinaitwa persistent grin
3.Misuli kukamaa na kuparalize au kupooza katika maeneo ya shingoni
4. Kupata shida sana ya kumeza kitu
5. Misuli ya tumboni kuwa migumu sana
6. Kukua kwa ugonjwa wa pepopunda husababisha maumivu yanayojirudia, pamoja na mgonjwa kupata mshtuko ambao hudumu kwa dakika kadhaa (spasms).
7. Kwa Kawaida, shingo na upande wa nyuma pamoja na miguu huwa migumu, mikono hunyooka kwa mbele huku ngumi zimekunjwa.
8. Ugumu wa misuli kwenye shingo na tumbo unaweza kusababisha shida ya kupumua.
• Kadri ugonjwa unavyoendelea, ishara zingine na dalili zinaweza kuonekana kama vile;
1. Shinikizo la damu kuwa juu au Mtu kuwa na Presha ya kupanda(High blood pressure)
2. Mapigo ya moyo kwenda mbio sana
3. Joto la mwili kuwa juu sana au mtu kuwa na Homa kali
4. Mgonjwa kuvuja Jasho sana mwilini
N.k
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!