Ni nini Husababisha Chuchu kupasuka hasa wakati wa kunyonyesha?

TATIZO LA CHUCHU KUPASUKA

• • • • • •

 Ni nini Husababisha Chuchu kupasuka hasa wakati wa kunyonyesha?


 -Chuchu zinaweza kukumbwa na matatizo mbali mbali kama vile:


• Kuwa na kidonda au kupasuka


 • Chuchu kutoa usaha au damu


 • Chuchu kuwasha n.k


 Ukweli ni kwamba katika hali ya kawaida Wanawake wengi wanaonyonyesha hawajui kunyonyesha kwa usahihi kama inavyotakiwa, huku wakikosea vitu vingi kama vile;


✓ Kutokuzingatia unyonyeshaji kwa muda wa kutosha kwa mtoto


✓  Kunyonyesha bila kufanya usafi wa matiti pamoja na chuchu


✓ Kukaa vibaya wakati wa unyonyeshaji pamoja na kumuweka mtoto vibaya wakati ananyonya n.k


BAADHI YA SABABU ZA CHUCHU KUPASUKA KWA MAMA ANAYENYONYESHA


- Kumuweka mtoto vibaya(poor positioning) wakati wa kunyonyesha hali ambayo hupelekea mtoto kuvuta chuchu kupita kiasi


- Mtoto kuwa na matatizo katika uumbaji ambayo huhusisha tatizo kwenye mdomo na ulimi kama vile; Tongue-tie,mdomo mdogo sana kuliko kawaida, kuwa na kidevu kidogo na kilichoshuka chini sana au kuingia ndani kuliko kawaida,tatizo la mdomo sungura(cleft lip and cleft palate),kuwa na Frenulum fupi n.k

 

Matatizo kama haya husababisha mtoto kubana chuchu kuliko kawaida wakati wa kunyonya,hali ambayo huweza kupelekea michubuko ya chuchu au vidonda.


 - Sababu zingine ni pamoja na:


• Tatizo la mtoto kushindwa kunyonya vizuri yaani poor sucking


• Tatizo la mtoto kuweka ulimi vibaya wakati wa kunyonya


• Tatizo la allergy


• Maambukizi ya magonjwa kwenye chuchu


• Mama kupaka vitu kama mafuta yenye kemikali flani ambayo huweza kusababisha ngozi ya chuchu kupasuka au kuwa na vidonda N.k


Ni muhimu sana kuchunguza na kufahamu chanzo cha tatizo hili, endapo ni vigumu kwako kujua,ongea na wataalam wa afya kwa ajili ya uchunguzi zaidi pamoja na Tiba.

 


KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.




0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!