Papa atoa wito wa kupiga Marufuku kubebewa Mimba

Papa atoa wito wa kupiga Marufuku kubebewa Mimba.

“Mtoto siku zote ni zawadi na sio msingi wa mkataba wa kibiashara.”

Papa Francis ametoa wito wa kupigwa marufuku hatua ya wanawake kukubali kubeba na kuzaa mtoto kwa niaba ya mtu mwingine au wanandoa ‘Surrogacy’ na kuita kitendo hicho kuwa “cha kusikitisha” katika hotuba yake huko Vatican siku ya Jumatatu.

“Ninaona tabia ya kusikitisha ya kile kinachoitwa uzazi wa ‘surrogate’ ambayo inawakilisha ukiukwaji mkubwa wa utu wa mwanamke na mtoto,” Papa alisema.

Papa Francis alisema anaimani kwamba jumuiya ya kimataifa itafanya jitihada za “kupiga marufuku tabia hii duniani kote.”

#papafrancis #vatican #uzazi #wajawazito

0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!