Ticker

6/recent/ticker-posts

Ugonjwa wa epididymitis,chanzo,dalili na Tiba yake



Ugonjwa wa epididymitis,chanzo,dalili na Tiba yake

Epididymitis ni tatizo linalohusisha kuvimba kwa mrija uliojikunja sehemu ya nyuma ya korodani ambao kwa kitaalam hujulikana kama epididymis.

Mrija huu kazi yake kubwa ni kuhifadhi na kubeba mbegu za kiume. Mwanaume wa umri wowote ndyo anaweza kupata tatizo la Epididymitis.

Dalili za Ugonjwa wa epididymitis

Mwanaume mwenye tatizo la Epididymitis anaweza kupata dalili kama hizi;

– Kupata joto,kubadilika rangi na Kuvimba kwa ngozi au kifuko cha korodani(Scrotum)

– Kupata maumivu ya korodani,ambapo mara nyingi huwa ya upande mmoja

– Kuumia wakati wa kukojoa

– Kupata hisia na kukojoa mara kwa mara

– Kutokwa na Uchafu kwenye Uume

– Kupata maumivu chini ya tumbo au eneo la via vya Uzazi

– Kutoa damu kwenye mbegu za kiume(kumwaga maji maji na shahawa zenye damu wakati wa tendo)

– Mara chache, kwa baadhi ya Wanaume hupata Homa.

Je, UTI inaweza kusababisha epididymitis? Soma hapa kufahamu Chanzo chake

Chanzo cha Ugonjwa wa epididymitis

Tatizo la Epididymitis huweza kusababishwa na;

1. Magonjwa ya Zinaa(STIs).

Magonjwa ya Zinaa kama vile Kisonono na chlamydia ni chanzo kikubwa cha tatizo la epididymitis

2. Maambukizi mengine.

Bacteria kutoka kwenye njia ya Mkojo au maambukizi kwenye Tezi dume(prostate) huweza kusambaa kutoka eneo la maambukizi hadi kwenye epididymis.

Pia maambukizi ya Virusi kama vile mumps virus, huweza kusababisha tatizo la epididymitis.

3. Mkojo kuingia kwenye mrija wa epididymis.

Hali hii hutokea pale ambapo mkojo hutiririka kwakurudi nyuma kisha kuingia kwenye mrija huu.

4. Kuumia(Trauma).

Kupata jeraha au kuumia eneo la Korodani huweza kusababisha tatizo la epididymitis.

5. Kupata ugonjwa wa Kifua kikuu au TB(Tuberculosis).

Kuna kesi chache pia tatizo la epididymitis husababishwa na maambukizi ya TB, japo hii ni nadra sana kutokea.

Vitu hivi huongeza hatari ya kupata Ugonjwa wa epididymitis

– Aina yoyote ya kufanya mapenzi ambayo huongeza hatari ya kupata magonjwa ya Zinaa-STIs hukuweka kwenye hatari ya kupata tatizo la epididymitis, mfano:

  • Kufanya mapenzi na mtu mwenye ugonjwa wowote wa Zinaa
  • Kufanya mapenzi bila kinga/condomu
  • Kufanya mapenzi kinyume na maumbile(Anal Sex) n.k
  • Kuwa na historia ya kuugua magonjwa ya Zinaa mara kwa mara

–  Kuwa na maambukizi kwenye njia ya Mkojo(UTI)

– Kuwa na maambukizi ya Tezi dume(prostate infection)

– Kufanyiwa huduma yoyote ya kitabibu ambayo hugusa njia ya Mkojo kama vile;Kuwekewa mpira wa mkojo(Urinary catheter) n.k

– Mwanaume kutokutahiriwa au kutokufanyiwa tohara

#SOMA hapa; Faida Zaidi za Mwanaume kufanyiwa Tohara

– Kukua kwa Tezi dume, ambapo huongeza hatari ya Mwanaume kupata maambukizi kwenye kibofu cha mkojo pamoja na tatizo la Epididymitis

– Kuwa na Matatizo mengine ambayo hudhoofisha kinga ya mwili kama vile HIV/AIDS n.k.

Madhara ya Ugonjwa wa epididymitis

Ukipata tatizo la epididymitis unaweza kupata madhara haya;

• Kupata jipu kwenye eneo la kifuko cha Korodani-Scrotum

• Maji au fluid kujikusanya kuzunguka korodani na kusababisha tatizo la hydrocele

• Kupata tatizo la Epididymo-orchitis, ikiwa tatizo la kuvimba kwa mrija wa epididymis limesambaa hadi kwenye Korodani.

• Pia kwa Kesi chache, hupunguza uwezo wa Mwanaume kumpa mimba mwanamke.

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.