Ciprofloxacin inatibu magonjwa gani,Soma hapa kufahamu
Ciprofloxacin inatibu nini?
Ciprofloxacin ni dawa jamii ya fluoroquinolone antibiotic ambayo hutumika kutibu aina mbali mbali za maambukizi ya bacteria.
Dawa ya Ciprofloxacin ipo kwenye kundi la quinolone antibiotics na huweza kutibu maambukizi ya bacteria kwa kuzuia ukuaji wao,
Kumbuka; Ciprofloxacin inatibu maambukizi ya bacteria pekee,haiwezi kufanya kazi kwa vimelea wengine wa magonjwa kama vile Virus,
Kutumia antibiotic yoyote wakati haihitajiki kunaweza kusababisha kutofanya kazi kwa maambukizi ya baadaye.
Kwa baadhi ya maambukizi, Ciprofloxacin hutumiwa pamoja na antibiotics zingine.
Dawa ya Ciprofloxacin Inaweza kutumika kama;
- kidonge kwa njia ya mdomo,
- kama matone ya jicho(eye drops),
- kama matone ya sikio(ear drops),
- au kwa njia ya mishipa(intravenously)
Ciprofloxacin inatibu magonjwa gani,Soma hapa kufahamu
Ciprofloxacin inatibu;
1. Ugonjwa wa UTI, au maambukizi ya bacteria kwenye njia ya mkojo
2. Maambukizi ya bacteria kwenye mifupa na joints(bone and joint infections),
3. Maambukizi ya bacteria ndani ya tumbo(intra-abdominal infections),
4. Aina kadhaa za magonjwa ya kuhara au infectious diarrhea,
5. Maambukizi ya bacteria kwenye mfumo wa hewa(respiratory tract infections),
6. Maambukizi ya bacteria kwenye ngozi(skin infections),
7. Ugonjwa wa homa ya matumbo(typhoid fever), n.k
SIDE EFFECTS ZA DAWA YA CIPROFLOXACIN
Baada ya kuitumia,Dawa ya Ciprofloxacin huweza kusababisha maudhi madogo madogo(side effects) ikiwemo;
- Kuhisi kichefuchefu
- Kuharisha
- Kupata kizunguzungu
- Kupata maumivu ya kichwa
- Au shida ya kulala inaweza kutokea.
Ikiwa yoyote ya athari hizi hudumu kwa muda mrefu au inakuwa mbaya zaidi, mwambie daktari wako au mfamasia mara moja ili kupata msaada wa haraka.
TAHADHARI JUU YA MATUMIZI YA Dawa ya Ciprofloxacin
- Kabla ya kutumia Dawa ya Ciprofloxacin, mwambie daktari wako au mfamasia ikiwa una mzio au allergy nayo,
- Au ikiwa una allergy na dawa zingine jamii ya quinolone antibiotics kama vile;
- norfloxacin,
- gemifloxacin,
- levofloxacin,
- moxifloxacin,
- Au ofloxacin;
- au ikiwa una mzio mwingine wowote. Dawa hii inaweza kuwa na viungo visivyotumika, ambavyo vinaweza kusababisha athari ya mzio au matatizo mengine. Zungumza na mfamasia wako kwa maelezo zaidi.
- Epuka kunywa kiasi kikubwa cha vinywaji vyenye kafeini kama vile kahawa, chai n.k
kula kiasi kikubwa cha chokoleti, au kuchukua bidhaa za dukani ambazo zina kafeini. Dawa hii inaweza kuongeza athari zaidi au kuongeza muda zaidi wa athari za kafeini.
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA JUU YA TATIZO LOLOTE TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.