Ticker

6/recent/ticker-posts

je unaweza kupata ukimwi bila kuchubuka



 je unaweza kupata ukimwi bila kuchubuka

HIV ni nini?
ni ufupisho wa Human Immunodefeciency Virus yaani virusi vinavyoua kinga ya mwili.HIV ni kirusi kinachoharibu uwezo wa mwili wako wa kujihami dhidi ya maambukizi.

AIDS ni ufupisho wa Acquired Immunodefeciency Syndrome, Tatizo la Upungufu wa Kinga Mwilini.

Watu wengi hufikiria kwamba watu ambao wana virusi hivyo, wana Ukimwi, ukweli ni kwamba virusi vya HIV ndivyo vinavyosababisha Ukimwi, yaani yawezekana mtu akawa na virusi vya ukimwi kwa muda mrefu bila ya kuugua ukimwi.

Hii inamaanisha Mtu anaweza kuwa na HIV bila kujua, wala kuona dalili zozote – Wakati huo iwapo tahadhari hazitachukuliwa anaweza kumwambukiza mtu mwengine .

Ukimwi ni nini?
Neno Ukimwi lina maana ya Ukosefu wa Kinga Mwilini. Hapa virusi vya HIV huwa vimeshambulia kinga ya aliyeambukizwa kiasi kuwa, mwili wake hauwezi tena kujipa ulinzi dhidi ya maambukizi.

Hivyo huonyesha dalili za magonjwa tofauti tofauti na hata saratani, hapo ndipo inasemekana kwamba wana ukimwi. Wakati huo ndipo kinga yao ya mwili huwa ni dhaifu sana,

na magonjwa nayo yanawashambulia kwa urahisi zaidi na yanakuwa vigumu kuyatibu,ndipo hapo ukimwi unasababisha kifo.

Fahamu kuwa kila mtu hukumbana na viini ambavyo husababisha magonjwa, lakini kama kinga yako ni imara si rahisi kupata maambukizo na hata ukipata ni rahisi kuyatibu lakini kwa wale waishio na virusi vya ukimwi kinga yao huwa imedhoofishwa sana kiasi kuwa akikumbana na viini ni rahisi kwake kupata maradhi na hata akitibiwa inachukua mda kupona.

JE UNAWEZA KUPATA UKIMWI BILA KUCHUBUKA?

Unaweza kupata VVU tu kwa kugusana moja kwa moja na majimaji/viowevu(fluids) fulani vya mwili kutoka kwa mtu aliye na VVU ambaye ana kiwango cha virusi kinachotambulika. Viowevu hivi ni pamoja na;

✓ Damu(Blood)

✓ Shahawa (cum) na maji kabla ya mbegu za kiume (pre-cum)

✓ Majimaji ya rectum(Rectal fluids)

✓ Majimaji ya ukeni(Vaginal Fluids)

✓ Maziwa ya mama

KUMBUKA: Ili maambukizi haya yatokee, Virusi vya UKIMWI katika viowevu hivi nilivyovitaja, lazima viingie kwenye mkondo wa damu wa mtu asiye na VVU kupitia utando wa mucous (unaopatikana kwenye puru, uke, mdomo, au ncha ya uume),

kwa kupitia njia mbali mbali kama vile kwenye vidonda, baada ya kuchomwa na vitu vya ncha kali kama sindano,nyembe n.k

HIVO UNAWEZA KUWA KWENYE HATARI ZAIDI YA KUPATA UKIMWI KWA NJIA HIZI

Hizi ndyo baadhi ya njia ambazo mtu huweza kuwa kwenye hatari zaidi ya kupata maambukizi ya UKIMWI;

- Kwa Kufanya ngono zembe au bila kinga kama Condom

- Kuwa na Wapenzi wengi,Multiple Sexual partners

- Kwa Kuchangia vitu vya ncha kali kama sindano,wembe,pini n.k na mtu aliyeathirika

- Mama aliyeambukizwa anaweza kumwambukiza mwanawe wakati wa uja uzito, kuzaa au kunyonyesha.

- Kuchangamana kwa damu au majimaji mengine ya mwili – mfano damu iliyo na virusi ikipenya kwenye jeraha au mchubuko.

- Kuongezewa damu iliyo na virusi N.k

HUWEZI KUAMBUKIZWA VIRUSI KUPITIA:

- kuamkiana kwa kushikana mikono.

- Kutumia kwa pamoja vifaa vya kulia chakula kama sahani,vijiko n.k

- Kukohoa au kwenda chafya.

- Kuumwa na wadudu kama kunguni au mbu au wanyama.

- Kula chakula kilichotayarishwa na mtu aliye na virusi vya ukimwi.N.k