Madhara ya kutoa mimba
Wanawake wengi huanza kukutana na matatizo haya baada ya kutoa Mimba;
– Kuvuja damu sana na kwa muda mrefu
– Kupata maumivu ya tumbo mara kwa mara, tumbo kukaza n.k
– Kupata shida ya kizunguzungu au hata kuzimia
– Kupata kichefuchefu na kutapika n.k
Dalili hizi huweza kuisha zenyewe ndani ya wiki ila wakati mwngine huweza kuwa tatizo la Muda mrefu.
Madhara ya kutoa mimba changa
Haya hapa ni Madhara ambayo huweza kutokea kwa Mtu kutoa Mimba;
1. Kuharibika kwa Kizazi au shingo ya kizazi(womb/cervix)
2. Kupata tatizo la kuvuja damu kupita kiasi
3. Mimba kutoka na kuacha mabaki mengine ndani(Incomplete abortion),
Hali hii ni ya hatari na inaweza kuleta madhara zaidi, hivo hatua za haraka ni muhimu,
Hii huweza kusababisha hata hatua kama (surgical abortion procedure) kufanyika.
4. Kupata maambukizi ya kizazi au mirija ya kizazi(uterus/fallopian tubes)
5. Kusababisha kovu au makovu ndani ya Kizazi
6. Kukuweka kwenye hatari Zaidi ya kupata maambukizi ya bacteria ambayo huingia moja kwa moja kwenye damu, na kisha kuleta madhara makubwa zaidi(Sepsis/Septic shock)
7. Kusababisha tatizo la kutoboka kwenye kizazi(Uterine perforation)
8. Utoaji Mimba Pia unaweza Kusababisha KIFO. n.k
Kwa Mujibu wa NCBI;
Zaidi ya asilimia 2% ya Wanaotoa Mimba hupata Matatizo kama vile;
- Kupata Maumivu makali ya Tumbo
- Kuvuja damu sana
- Maambukizi ya magonjwa n.k
Utafiti wa NCBI unaendelea Kuonyesha; Na wengine hupata Madhara makubwa ikiwemo;
– Tatizo la misuli ya kizazi kushindwa kurudi mahali pake,tatizo ambalo kitaalam hujulikana kama uterine atony
– Kuvuja damu mvululizo(Subsequent hemorrhage)
– Kutoboka kwa Kizazi(uterine perforation),
– Kuumia kwa viungo vya karibu na kizazi kama vile; kibofu cha Mkojo au eneo la haja kubwa(injuries to adjacent organs (bladder or bowels),
– Kuchanika kwa mlango wa kizazi(cervical laceration),
– Mimba kushindwa kutoka, na kuleta madhara Zaidi(failed abortion),
– Kupata maambukizi hatari ya bacteria kwenye damu baada ya kutoa mimba( septic abortion)
– Kupata matatizo ya damu kuganda:disseminated intravascular coagulation.n.k
Kadri Mimba inavyokuwa kubwa Zaidi ndivyo hatari na madhara huongezeka Zaidi.
Maambukizi kwenye eneo la Via vya Uzazi(Pelvic Infection):
Bakteria (vijidudu) kutoka kwenye uke au mlango wa uzazi wanaweza kuingia kwenye uterasi na kusababisha maambukizi.
Matumizi ya Antibiotics yanaweza kusaidia kuondokana na maambukizi hayo.
Mimba kushindwa kutoka kabsa(Incomplete abortion):
Mabaki ya ujauzito kubaki ndani ya kizazi hali ambayo ni hatari Zaidi na huhitaji matibabu ya haraka.
Pia Utoaji mimba usio kamili unaweza kusababisha maambukizi na kutokwa na damu Zaidi.
Damu kuganda na kutengeneza Blood clots ndani ya kizazi:
Shida hii huweza kusababisha maumivu makali ya tumbo, lakini hatari zaidi ya kupoteza maisha, baada ya blood clots kusafiri kwenye damu mpaka kwenye mapafu na Kuziba.
Kuvuja damu kupita Kiasi:
Kutokwa na damu nyingi sio kawaida na kunaweza kusababisha madhara Zaidi.
Kuchanika kwa Mlango wa kizazi(cervix):
Kutoboka kwa kuta za kizazi(Perforation of the uterus wall:
Kifaa cha matibabu kinaweza kupitia ukuta wa uterasi na kutoa.Kwa Mujibu wa NCBI;
Kiwango kilichoripotiwa ni moja(1) kati ya kila utoaji mimba 500. Kulingana na ukali, utoboaji unaweza kusababisha maambukizi, kutokwa na damu nyingi au vyote viwili. Upasuaji unaweza kuhitajika ili kurekebisha tishu za uterasi, na katika hali mbaya zaidi kutoa kizazi chochote au hysterectomy inaweza kuhitajika.
Madhara Mengine ya Muda mrefu ya Kutoa Mimba ni pamoja na;
- Mwanamke Kushindwa kubeba Mimba tena
- kuwa kwenye hatari ya kupata Saratani za matiti,Ovari au kizazi(breast, ovarian and endometrial cancer).
Kupata madhara kisaikolojia(Emotional Side of an Abortion)
Unapaswa kujua kwamba wanawake hupata hisia tofauti baada ya kutoa mimba, Baadhi ya wanawake wanaweza kujisikia hatia, huzuni au kuwa na Msongo wa mawazo ambao hauishi baada ya kutoa Ujauzito,
wakati wengine wanaweza kuhisi utulivu kwamba utaratibu umekwisha. Baadhi ya wanawake wameripoti madhara makubwa ya kisaikolojia baada ya kutoa mimba, ikiwa ni pamoja na;
- mfadhaiko,
- huzuni,
- wasiwasi,
- kujidharau
- majuto,
- Woga
- kurudi nyuma kwa kila kitu anchofanya
- na kuingia kwenye matumizi mabaya ya dawa za kulevya.
Hisia hizi zinaweza kuonekana mara baada ya utoaji mimba au hatua kwa hatua kwa muda mrefu. Hisia hizi zinaweza kujirudia au kuhisiwa kuwa na nguvu zaidi wakati wa utoaji mimba mwingine, au kuzaa kwa kawaida, au siku ya kumbukumbu ya utoaji mimba.
Ushauri au usaidizi kabla na baada ya kutoa mimba ni muhimu sana. Ikiwa haupati msaada na utegemezo wa familia, huenda ikawa vigumu kwako kukabiliana na hisia zinazotokea baada ya kutoa mimba.
Kuzungumza na mshauri wa kitaalamu kabla ya kutoa mimba kunaweza kumsaidia mwanamke kuelewa vyema uamuzi wake na hisia anazoweza kupata baada ya utaratibu huu.
Ikiwa ushauri nasaha haupatikani kwa mwanamke, hisia hizi zinaweza kuwa ngumu zaidi kushughulikia. Vituo vingi vinavyohusika na kesi za ujauzito hutoa huduma za ushauri kabla na baada ya kutoa mimba.