MENO YA PLASTIC KWA WATOTO(Chanzo na matibabu yake),NATAL TEETH/BABY TEETH
Meno ya plastic ni meno ambayo mtoto anazaliwa nayo, meno haya kwa lugha nyingine hujulikana kama Natal Teeth, na wengine huita baby teeth.
KUMBUKA:
(i) Meno ambayo mtoto huzaliwa nayo ndyo huitwa meno ya plastic, Natal Teeth au Baby teeth
(ii) Meno ambayo huota kwenye hatua za kawaida za ukuaji wa mtoto huitwa neonatal teeth
Sio watoto wengi sana wanakuwa na meno haya, ila wapo baadhi ya watoto ambao huzaliwa tayari wana meno haya,
Meno haya ambayo mtoto huzaliwa nayo hayana madhara yoyote kwa mtoto, japo wakati mwingine huweza kuleta shida kwa Mama wakati mtoto ananyonya.
CHANZO CHA MENO YA PLASTIC KWA WATOTO
Meno haya nitofauti na meno ya kawaida(not fully developed),na pia hayana mizizi imara kama meno mengine.
Meno haya sio sawa na meno ambayo huanza kuota kwenye hatua za ukuaji wa mtoto yaani neonatal teeth,
Na mpaka sasa hakuna sababu ya moja kwa moja ambayo imegundulika kama chanzo rasmi cha kuota meno haya ya plastic.
MATIBABU YA MENO YA PLASTIC
Huhitaji kuhangaika na matibabu yoyote juu ya meno haya, japo unaweza kuongea na wataalam wa afya kwanza,wamuone na kumchunguza mtoto wako.
Meno haya hayana madhara yoyote kwa Mtoto wako, lakini kwa baadhi ya wataalam wa afya wanaweza kushauri yaondolewe kama yamesababisha tatizo lolote.