Ugonjwa Wa Mpox,chanzo,dalili Na Tiba yake
Ugonjwa wa homa ya nyani au Mpox ni ugonjwa ambalo unasababishwa na virusi, Ugonjwa huu unasababishwa na virusi ambao hujulikana kwa jina la Mpox ambapo hapo awali vilijulikana kama MonkeyPox. Mpox Virus wapo kwenye kundi la Orthopoxvirus genus ndani ya familia ya Poxviridae.
Ugonjwa wa homa ya nyani kwa binadamu(Human Mpox),Mara ya kwanza kabsa uliripotiwa Mwaka 1970 nchini DRC(Democratic Republic of the Congo) kwa kijana mmoja wa Miaka 9 aliyekuwepo kwenye eneo ambalo ugonjwa wa Smallpox ulishaondolewa tangu mwaka 1968. Ndipo visa vingine vikaanza kuripotiwa na maeneo mengine, (Disease history Source:WHO)
Dalili za Mpox
DALILI ZA UGONJWA HUU WA MPOX NI PAMOJA NA;
– Mtu kuwa na homa pamoja na mwili kutetemeka
– Kupata maumivu makali ya kichwa
– Mwili kuchoka kupita kawaida
– Mwili kukosa nguvu na kuwa dhaifu sana
– Lymph nodes kuanza kuvimba ambapo kwa lugha nyingine hujulikana kama lymphadenopathy
– Kupata maumivu ya viungo,joints pamoja na misuli ya mwili
– Kupata maumivu ya mgongo(back ache)
– Kutokewa na UPELE kwenye maeneo mbali mbali ya mwili wako kama vile; Usoni, kwenye mikono pamoja na viganja vya mikono,
miguuni,machoni,,mdomoni,sehemu za siri n.k
Upele huu unaweza kuwasha sana, na hata baadae huweza kutumbuka kabsa,
Mwili huweza kubaki na makovu au alama alama.
UGONJWA HUU WA HOMA YA NYANI(MPOX) husambaa kutokana na ukaribu(Close contact) kwa mtu,wanyama au vitu ambavyo tayari vina virusi hawa wa Mpox.
Unaweza kuupata kwa njia ya ya mgusano sehemu zenye majeraha, kupitia body fluids zote kama vile damu,mate,jasho n.k, kutoka kwa Mtu au wanyama wenye Virusi hawa(Mpox virus).
Virusi vya MPox vinaweza kuingia mwilini kupitia kwenye ngozi iliyo na jeraha au michubuko yoyote, au kwa njia nyingine kama vile njia ya upumuaji au kupitia macho, pua pamoja na mdomo.
Pia Uenezwaji wake unaweza kuwa kwa kugusana na wanyama walioambukizwa kama vile nyani, panya na kindi ,kupitia vitu kama vile matandiko au nguo za mgonjwa mwenye virusi hawa.
🟩 Ugonjwa wa Mpox unaweza kusambaa kutoka kwa mtu mwenye maambukizi kwenda kwa mwingine kwa njia zifuatazo; kupitia maji maji ya mwili ikiwemo mate, matapishi, jasho, mkojo, matone ya mfumo wa njia ya hewa na ngozi kupitia kugusana na kujamiana na mtu mwenye maambukizi ama kutumia vifaa, matandiko au kugusa sehemu zilizo na vimelea vya ugonjwa huu. Aidha, ugonjwa huu unaweza pia kuenezwa kutoka kwa wanyama kwenda kwa binadamu.
🟩 Dalili kuu ya Mpox ni upele, malengelenge au vidonda kwenye mwili hasa, mikono na miguu, kifuani, usoni na wakati mwingine sehemu za siri. Dalili nyingine ni homa, uchovu, maumivu ya kichwa, misuli, mgongo, uchovu na kuvimba mitoki.
🟩 Ugonjwa huu haujaingia nchini, hivyo, ni vyema tukashirikiana kuhakikisha nchi yetu inabaki kuwa salama. Wizara inatoa tahadhari kwa Wananchi wote kuchukua hatua za kujikinga na ugonjwa wa huu kwa kutekeleza yafuatayo;-
i. Kutoa taarifa kupitia namba 199 bila malipo endapo utamuona mtu mwenye dalili za Mpox.
ii. Kuepuka kugusa majimaji ya mwili au ngozi ya mtu mwenye dalili za ugonjwa wa Mpox.
iii. Kuepuka kusalimiana kwa kupeana mikono, kukumbatiana na kubusiana mtu mwenye dalili za Mpox.
iv. Kuepuka kugusana na mtu yeyote mwenye dalili za ugonjwa wa Mpox.
v. Kunawa mikono kila mara kwa maji tiririka na sabuni au kutumia vitakasa mikono.
vi. Epuka kula au kugusa mizoga au wanyama mfano nyani au swala wa msituni.
vii. Safisha na kutakasa vyombo vilivyotumika na mhisiwa au mgonjwa pamoja na maeneo yote yanayoguswa mara kwa mara.
viii. Kuvaa barakoa iwapo itabidi kukaa na kuongea kwa karibu na mtu mwenye dalili za Mpox.
ix. Kuwahi katika vituo vya huduma za afya unapoona dalili za ugonjwa wa Mpox.
x. Watoa huduma za afya kuzingatia miongozo ya kuzuia kusambaa kwa maambukizi (IPC) wakati wote wanapowahudumia wagonjwa.
Via:WizaraafyaTz
#SOMA Zaidi hapa kuhusu Ugonjwa wa Mpox
MATIBABU YA UGONJWA WA MPOX
Ugonjwa huu hauna tiba(no cure),bali watalaam wa afya hudhibiti dalili zinazotokana na ugonjwa huu wa homa ya nyani.
Hata hivo ugonjwa huu huisha wenyewe kwa kipindi flani baada ya kumpata mtu.
Fahamu pia,Maambukizi haya ya ugonjwa wa homa ya nyani(Mpox) huisha yenyewe na hudumu kati ya siku 14 na 21.
0 Comments