Tatizo La Kukosa Choo Chanzo Na Tiba yake
Tatizo la kukosa choo ni hali ambayo mtu anapata ugumu wa kujisaidia au hapati haja kubwa kwa siku kadhaa (mara nyingi chini ya mara 3 kwa wiki). Hali hii inaweza kuwa ya muda mfupi au ya kudumu kulingana na chanzo chake.
Kukosa choo au kupata choo kigumu(Constipation) ni tatizo linalotokea kwa Watu wengi, na baadhi ya Tafiti huonyesha kwamba huathiri karibu 20% ya watu kila mwaka (Cirino, 2019).
Na hapa ndani ya afyaclass tunapata Si chini ya wagonjwa 5 kwa Siku,kila Siku wenye changamoto ya aina hii, kwa kuliona tatizo hili jinsi ambavyo huendelea kusumbua watu wengi,tumeona umuhimu mkubwa wa kukuelimisha wewe.
Kama wewe ni Miongoni mwa Watu wenye Shida hii,Unahitaji kujua Sababu zake na nini cha kufanya ili uondokane na hali hii.
Tuangalie Sababu mbali mbali za Tatizo hili la kukosa Choo katika Makala Hii,,
Chanzo cha Tatizo la Kukosa Choo
Kuna sababu kadhaa zinazoweza kusababisha kukosa choo na Sababu Hizi ni pamoja na:
1. Kutokula vyakula vyenye nyuzinyuzi(fibers ndogo)
Baadhi ya Watu huweza kupata tatizo la kukosa choo kwa Sababu hawali vyakula vyenye nyuzinyuzi(fibers) za kutosha.
Tafiti nyingi huonyesha Kula vyakula vya nyuzinyuzi zaidi kunaweza kusaidia kupunguza au kuondoa tatizo hili la Kukosa Choo.
Mifano ya vyakula vya nyuzinyuzi kwa makundi ambavyo hupatikana kwenye jamii zetu ni pamoja na:
-Mboga za majani kama vile:
- Sukuma wiki
- Spinachi
- Mchicha
- Kabeji
- Ulaji wa Karoti n.k.
- Kula Matunda kama vile;
- Papai
- Tufaha (apple)
- Ndizi (hasa mbivu za kijani kidogo)
- Embe
- Tikiti maji
- Chungwa n.k
- Vyakula vya nafaka kama vile;
- Unga wa dona
- Ngano nzima
- Mahindi yasiyokobolewa
- Maharage na jamii zake
- Maharage ya kawaida
- Kunde
- Njugu
- Choroko
- Dengu
- Mbegu na karanga
- Mbegu za maboga
- Mbegu za alizeti
- Karanga n.k.
Fahamu kwamba; Kula vyakula vingi vya wanga vilivyosindikwa kama mikate meupe, wali mweupe, au viazi bila mboga huweza kuongeza hatari ya kupata tatizo hili.
2. Kutokunywa maji ya kutosha
Upungufu wa maji mwilini hufanya kinyesi kuwa kigumu na kigandamane, Lakini pia hukuweka kwenye hatari zaidi ya kukosa choo kabsa.
3. Matumizi ya baadhi ya Dawa
Baadhi ya dawa, ikiwa ni pamoja na dawa za maumivu au jamii ya opioids, baadhi ya dawa za Presha,Dawa za madini chuma n.k. zinaweza kupunguza usagaji chakula na kusababisha tatizo la kukosa choo.
Pia dawa jamii ya Antidepressants,Baadhi ya Antacids,antihistamines n.k..
4. Kuziba kwa njia ya haja kubwa
Tatizo hili pia linaweza kusababisha Mtu asipate choo kabsa.
5. Uwepo wa Magonjwa mbali mbali
Magonjwa kama vile Kisukari, matatizo ya tezi kama vile tatizo la hypothyroidism, ugonjwa wa koloni au utumbo mpana au Irritable bowel syndrome (IBS), au kuwa na saratani ya utumbo,Vyote hivi huweza kuchangia tatizo la kukosa choo.
Fahamu kwamba matatizo yote yanayosababisha Uharibifu wa neva mbalimbali katika njia ya usagaji chakula yanaweza kupunguza usagaji chakula, na kusababisha dalili hizi za kukosa choo kwa mgonjwa.
Majeraha ya neva, kama vile kwenye eneo la uti wa mgongo au majeraha ya ubongo, yanaweza pia kupunguza usagaji chakula, na kupelekea tatizo hili la kukosa choo kabsa.
6. Sababu zingine za kawaida ni pamoja na;
- Kukosa mazoezi
Mwili usiotembea au kufanya shughuli au mazoezi huchangia utumbo kufanya kazi taratibu, na hii huweza kuongeza hali hii ya kukosa choo
- Kuchelewesha haja kubwa mara kwa mara
Mtu akizoea kuzuia haja kubwa, misuli ya utumbo hupoteza msukumo wa kawaida, na huweza kuwa kwenye hatari ya kukosa choo pia.
- Mabadiliko ya Kimaisha
Kuwa na Msongo wa mawazo, ujauzito, au safari ndefu zinaweza kubadilisha mpangilio wa choo.
Zingatia Mambo haya Muhimu sana kwako
1. Fanya Mabadiliko ya lishe yako,Ongeza vyakula vyenye nyuzinyuzi kama vile:
Mboga za majani kama (sukuma, mchicha, kabichi)
Matunda (papai, embe, parachichi, ndizi mbivu)
Nafaka zisizosindikwa (mtama, ulezi, unga wa dona)
Epuka vyakula vya kukaanga sana na vyakula vya mafuta mengi.
2. Kunywa maji ya kutosha
Angalau glasi 6–8 za maji kila siku.
Maji ya uvuguvugu asubuhi yanaweza kusaidia kusisimua utumbo.
3. Fanya Mazoezi ya mwili
Kutembea kwa dakika 30 kila siku husaidia kuamsha utumbo na kuondoa hali hii ya kukosa choo.
4. Kuanzisha ratiba ya kwenda chooni
Jisaidie kila siku muda uleule, hasa baada ya kula.
5. Tiba ya dawa (ikiwa njia asili hazijasaidia)
Pata Dawa za kuondoa tatizo hili,Tumia dawa kwa ushauri wa daktari tu, kwani matumizi mabaya yanaweza kusababisha madhara zaidi.
Je,Una tatizo hili na hujapata Msaada wa Tiba?
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU NA TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
Rejea Sources:
- https://www.medicalnewstoday.com/articles/327136#causes
- https://my.clevelandclinic.org/health/diseases/4059-constipation
- https://cdhf.ca/en/constipation-what-to-do-if-you-cant-poop/#:~:text=Constipation%20is%20quite%20common%2C%20affecting,can%20indicate%20something%20is%20wrong.







.jpeg)
.jpeg)







image quote pre code