Uzito wa mtoto kulingana na umri,Soma hapa
Moja ya vitu muhimu ambavyo huangaliwa kwenye ukuaji wa mtoto ni pamoja na uzito wake,
Uzito ni kiashiria kimojawapo cha ukuaji kwenye mwili wa mtoto. Watoto hukua kwa kasi tofauti, lakini chati za ukuaji zinaweza kutoa mwongozo kuhusu kiwango cha Uzito wa mtoto ambacho anapaswa kuwa nacho kwa wastani kulingana na umri wake.
Wastani wa Uzito wa Mtoto kwa Mwezi
Kwanza, ni muhimu kuzingatia kwamba uzito wa wastani kwa mtoto sio uzito "wa kawaida" kama watu wazima, watoto wachanga huzaliwa kwa maumbo na saizi mbali mbali.
Vivyo hivo wakati mwingine Ikiwa uzito wa mtoto uko katika asilimia za chini, hii haimaanishi ana shida kwenye ukuaji wake, Kwa kuzingatia hili, kutumia chati ya uzito kunaweza kumsaidia mtu kufuatilia ukuaji wa mtoto wake kwa ujumla.
Vituo vya Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa (CDC) vinapendekeza kutumia chati ya uzito ya Shirika la Afya Duniani(WHO) kwa watoto hadi umri wa miaka 2.
Makala hii inaelezea uzito wa wastani kwa mtoto "mwezi hadi mwezi" tangu kuzaliwa. Pia inachunguza kile kinachoweza kuathiri uzito wa mtoto.
Kulingana na WHO, wastani wa uzito wakati wa kuzaliwa kwa mtoto wa kiume aliyezaliwa muda kamili "full-term" ni kilo 3.3 (kg),
Wakati Uzito wa wastani wakati wa kuzaliwa kwa mtoto wa kike aliyezaliwa muda kamili ni kilo 3.2(kg),
Na Uzito wa wastani kwa mtoto aliyezaliwa kati ya wiki 37-40 ni kilo 2.5 hadi 4.
NB: Wakati wa kuzaliwa, Mtoto huwa na tatizo la Uzito mdogo(low-birth weight) endapo amezaliwa akiwa na Uzito wa chini ya Kilogram 2.5 kg.
Ni kawaida kwa watoto kupoteza takriban asilimia 10% ya uzito wao punde tu baada ya kuzaliwa. Kupungua huku kunatokana zaidi na upotezaji wa maji na kwa kawaida hakuna kitu cha kuwa na wasiwasi kuhusu hili. Watoto wengi hurejesha uzito huu ndani ya wiki 1.
Chati ya uzito wa mtoto kwa umri(Baby weight chart by age)
Chati hizi za Uzito zinaweza kumsaidia mtu kujua ni asilimia ngapi ya uzito wa mtoto wake. Kwa mfano, ikiwa uzito wake uko katika asilimia 60%, inamaanisha kwamba asilimia 40% ya watoto wa umri sawa na wake pamoja na jinsia sawa na yake wana uzito zaidi, na asilimia 60% ya watoto hawa wana uzito mdogo.
Chati iliyopo hapa chini inaonyesha uzito wa watoto katika asilimia 50(50th percentile),
Hii ni uzito wa wastani. Watoto wa kiume huwa na uzito mkubwa kidogo zaidi ya watoto wa kike, hivyo chati hii imegawanywa kulingana na jinsia ya mtoto.
UZITO/KE FemaleTrusted Source 50th percentile
UZITO/ME MaleTrusted Source 50th percentile weight
UMRI | UZITO/KE | UZITO/ME |
Kuzaliwa | (3.2 kg) | (3.3 kg) |
1 mwezi | (4.2 kg) | (4.5 kg) |
2 miezi | (5.1 kg) | (5.6 kg) |
3 miezi | (5.8 kg) | (6.4 kg) |
4 miezi | (6.4 kg) | (7.0 kg) |
5 miezi | (6.9 kg) | (7.5 kg) |
6 miezi | (7.3 kg) | (7.9 kg) |
7 miezi | (7.6 kg) | (8.3 kg) |
8 miezi | (7.9 kg) | (8.6 kg) |
9 miezi | (8.2 kg) | (8.9 kg) |
10 miezi | (8.5 kg) | (9.2 kg) |
11 miezi | (8.7 kg) | (9.4 kg) |
12 miezi | (8.9 kg) | (9.6 kg) |