HOSPITALI ZOTE NCHINI ANZENI KUTUMIA SIMU ZA UPEPO
Na WAF - Dar Es Salaam
Waziri wa Afya Mhe. Jenista Mhagama amezitaka Hospitali zote nchini kuanzisha mfumo wa matumizi ya simu za upepo ili kupunguza matumizi ya siku za mkononi ambazo hazina tija kwenye utoaji wa huduma bora kwa wananchi.
Waziri Mhagama ameyasema hayo leo Septemba 12, 2024 jijini dodoma wakati wa uzinduzi wa miradi na matukio katika Hospitali ya Benjamin Mkapa jijini Dodoma.
Amesema simu hizo zitasaidia uwajibikaji wa watumishi wa sekta ya afya na kugundua utoro kwa watumishi wasiohudhuria kazini.
“Mfumo huu ni mzuri sana hongereni kwa ubunifu nitumie fursa hii kuagiza hospitali zote nchini kuanzisha na kutumia mfumo huu ambao utasaidia kubaini utoro kwa watumishi”
Waziri Mhagama ameupongeza uongozi wa Hospitali hiyo kwa ubunifu huo mzuri na utoaji wa huduma bora kwa wateja kupitia mbinu za kuhakikisha wanawahudumia wagonjwa kwa ufanisi na kuleta tija.
Wakati huo huo.Mhe. Mhagama amesema kuwa Magari matatu ya upasuaji aliyoyazindua yanalengo la kutoa huduma za kibingwa za upasuaji kwa watanzania hususan ni hospitali zilizopo pembezoni mwa nchi ambazo hazina vyumba vya kufanyia huduma husika.
“Magari haya yatatumika kwa miezi mitatu yatasaidia kuwafikia wananchi wengi ambao wako katika maeneo yasiyo na vyumba vya upasuaji na kuondoa gharama za matibabu na kutoa mafunzo katika hospitali hizo magari hayo yataweza kuimarisha tiba utalii na kuitangaza Tanzania.